Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 16, 2025 Local time: 08:09

Macron kutangaza hatua mpya kukabiliana na maadamano yanayo endelea Ufaransa


Waandamanaji wakikabiliana na vyombo vya dola Ufaransa Desemba. 8, 2018.
Waandamanaji wakikabiliana na vyombo vya dola Ufaransa Desemba. 8, 2018.

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa anatazamiwa kutangaza hatua mpya za kuwaridhisha waandamanaji wa Koti manjano hivi punde atakapo lihutubia taifa.

Hatua hizi mpya zinakuja kufuatia maandamano na ghasia za wiki tatu zilizoathiri uchumi wa nchi hiyo.

Maafisa wa serikali wanakiri kwamba hawakutarajia kuwa watu wanahasira kwa kiwango hicho na kuwa patakuwa na maandamano yatakayo dumu kwa wiki tatu, kutokana na hali ngumu ya maisha.

Mapema Jumatatu kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 40, anaekabiliwa na wito kutoka wanasiasa wa pande zote kufanya mabadiliko makubwa, alikutana na baraza lake la mawaziri kwa kikao cha dharura kuzungumzia hatua zinazopasa kuchukuliwa.

Waziri wa Fedha Bruno Le Marie anasema ghasia za wiki kadhaa zimesababisha hasara kubwa katika uchumi; ikiwemo utalii na viwanda.

Macron amelazimika kubadili msimamo wake baada ya karibu watu laki tatu kujitokeza tena katika mji mkuu, Paris, siku ya Jumamosi wakiandamana kumtaka kiongozi huyo ajiuzulu.

Wakuu wa Paris wanasema waandamanaji wamesababisha hasara kubwa kwa kuvunja maduka na kupindua magari ya umma na watu binafsi.

Maandamano hayo yaliyo anza mwezi uliyopita kupinga kupandishwa kodi ya mafuta ya diazeli ili kupunguza uchafuzi wa hewa yamebadilika hivi sasa kulalamika dhidi ya kupanda kwa hali ya maisha kwa ujumla wakimlaumu Macron kutetea zaidi maslahi ya matajiri.

Waandamanaji hao hivi sasa miongopni mwa madai yao ni kuongezwa kwa kiwango cha chini cha mshahara jambo ambalo limepingwa na waziri wa kazi jana.

XS
SM
MD
LG