Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 20:33

Croatia, Ufaransa katika fainali Kombe la Dunia


Mario Mandžukić wa Croatia akisherehekea goli la ushindi dhidi ya Uingereza Jumatan\o.
Mario Mandžukić wa Croatia akisherehekea goli la ushindi dhidi ya Uingereza Jumatan\o.

Goli la Mario Mandzukic katika dakika za nyongeza limeiingiza Croatia katika fainali ya Kombe la Dunia baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Uingereza Jumatano. Croatia sasa itapambana na Ufaransa Jumapili mjini Moscow. Ufaransa iliingia fainali baada ya kuitoa Ubelgiji katika nusu fainali.

Uingereza ilipata goli zuri katika dakika za mwanzo tu za mechi dhidi ya Croatia kwa goli la Kieran Trippier katika dakika ya tano tu, na kwa muda mrefu wa kipindi cha kwanza Uingereza ilikuwa inaelekea katika fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1966.

Lakini Croatia walitumia vizuri utawala wao wa katikati ya uwanja huku mchezaji wao wa kiungo Luka Modric akisuka mashambulizi makali dhidi ya Uingereza.

Utamu wa kuingia fainali ya Kombe la Dunia
Utamu wa kuingia fainali ya Kombe la Dunia

​Baada ya kuhimili mashambulizi kutoka kila upande Uingereza walijikuta wakilizwa na Ivan Perisic alipokomboa kwa goli safi katika dakika ya 68.

Kuanzia hapo Uingereza ililazimika kulinda mlango wao kwa kila hali huku Croatia ikifanya mashambulizi makali hadi dakika 90 kumalizika. Uingereza mchezo wa kujihami katika dakika za nyongeza na ndipo Mandzukic alipoipatia Croatia bao la ushindi katiika dakika ya 109.

Hii ilikuwa mechi ya tatu mfululizo kwa Croatia kucheza dakika 120 baada ya kulazimishwa kuingia dakika za nyongeza katika mechi zake mbili zilizopita dhidi ya Russia, na Denmark kabla ya hapo.

Itakuwa mara ya kwanza Croatia kucheza katika mechi ya fainali ya Kombe la Dunia wakati Ufaransa wamerudi katika fainali baada ya kushinda kombe hilo mwaka 1998.

XS
SM
MD
LG