Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 18:38

Ufaransa : Zaidi ya watu 100 wamekamatwa, polisi, raia wajeruhiwa


Polisi wakitumia magari ya maji ya mwasho kuzuia maandamano nchini Ufaransa.
Polisi wakitumia magari ya maji ya mwasho kuzuia maandamano nchini Ufaransa.

Kwa mara nyingine tena waandamanaji wamejitokeza katika mtaa mkubwa maarufu Paris, Champ Elysees, na polisi kuendelea kutumia mabomu ya machozi, mabomu ya kutishia na maji ya mwasho Jumamosi dhidi ya waandamanaji hao waliokuwa wakivuka vizuizi vya usalama katika bara hiyo.

Maafisa wa polisi wamesema zaidi ya watu 100 wamekamatwa Jumamosi huko Paris, na shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa askari sita na waandamanaji 14 wamejeruhiwa.

Baadhi ya waandamanaji walikusanya kuni na mabaki ya ujenzi karibu na eneo la kumbukumbu maarufu la Arc de Triomphe na kuwasha vitu hivyo moto, polisi wamesema.

Ni mara ya tatu katika wiki kadhaa waandamanji wamejitokeza kuonyesha kero yao na kushinikiza kukoma kwa ongezeko la kodi hasa katika bidhaa za petroli, na kutaka kiongozi wa nchi hiyo Emmanuel Macron kusikiliza kero zao kwa kuandamana mitaani.

Waziri Mkuu Edouard Philippe amesema kuwa Edouard Philippe amesema kuwa polisi 5,000 walikuwa wamepelekwa maeneo mbalimbali ya jiji hilo la Paris ili kuwadhibiti waandamanaji hao.

XS
SM
MD
LG