Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Februari 04, 2023 Local time: 04:33

Ufaransa yafuzu raundi ya pili


Ushindi wa goli (1 – 0) dhidi ya timu ya Peru kutoka Amerika Kusini umeipeleka Ufaransa katika raundi ya pili ya mtoano katika Kombe la Dunia Russia 2018.

Ufaransa imefuzu kwa kuandikisha pointi 6 na kuwa kinara wa kundi C ikifuatiwa na Denmark yenye pointi 4.

Timu za Denmark na Australia itabidi kugombania nafasi moja iliyobaki katika kundi hilo. Denmark itahitaji pointi moja tu kusonga mbele, huku Australia ikiomba Ufaransa ishinde dhidi ya Denmark, na kuifunga Peru kwa zaidi ya goli 1.

Wachambuzi wa soka walikosoa kiwango cha Ufaransa katika mchezo wake na Australia, lakini kwa sasa wachambuzi wanasema ukweli ni kwamba michuano ya mwaka huu ina ushindani mkubwa.

Ufaransa sasa itaelekeza nguvu yake katika raundi ya pili ikisubiri kujua timu itakayokabiliana nayo. Timu yam waka huu inajumuisha wachezaji vijana wanaochezea vilabu vikubwa barani Ulaya.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG