Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 11:23

Macron ampa uraia kijana aliyemuokoa mtoto Ufaransa


Mamoudou Gassama
Mamoudou Gassama

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron yeye mwenyewe amemshukuru kijana mhamiaji Jumatatu katika Ikulu ya Elysee ambako Mamoudou Gassama, mwenye miaka 22, kutoka Mali amemwambia rais “Mungu alinisaidia” katika hatua yangu ya kumuokoa mtoto.

Amesema kuwa: “Kadiri nilivyokuwa naparamia ukuta, ndivyo nilivyozidi kupata ushujaa wa kuparamia ukuta huo juu zaidi.” Kutokana na hilo Gassama ameendelea kupongezwa na wengi kama shujaa.

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa hapo ndipo Spiderman wa kweli alipoingia kazini huko Paris na kumuokoa mtoto huyo wa kiume aliyekuwa ananing’inia kutoka katika balkoni ya ghorofa ya nne.

Mamoudou Gassama, mwenye umri wa miaka 22 kutoka Mali, amesema baada ya kuona mtoto huyo yuko hatarini katika eneo jirani ambako alikwenda kuangalia shindano la mpira wa miguu uliokuwa unaonyeshwa katika televisheni kwenye mgahawa mmoja.

Rais Macron ametangaza kuwa Gassama atatunukiwa uraia wa Ufaransa na kupatiwa kazi katika idara ya zimamoto.

Mayor wa Paris Anne Hildalgo amesema katika ujumbe wa Twitter kuwa alimpigia simu Gassama kumshukuru kwa kitendo chake cha ushujaa.

“Alinieleza kuwa aliwasili nchini kutoka Mali miezi michache iliyopita akiwa na ndoto ya kujitafutia maisha hapa. Nilimjibu kuwa kitendo chake cha ushujaa ni mfano kwa raia wote na kuwa Jiji la Paris litakuwa na hamu ya kumsaidia katika juhudi zake za kutaka kuishi Ufaransa,” ameposti katika Twitter.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, wazazi wa mtoto hawakuwa nyumbani wakati wa tukio hilo. Mama alikuwa nje ya mji na baba ya mtoto huyo amepangiwa kufika mahakamani Jumatatu baada ya kuhojiwa ni kwa sababu gani alimwacha mtoto peke yake.

Shujaa huyo ameiambia CNN, …” Ninapenda watoto. Ningeumia sana kumuona amejeruhiwa mbele yangu. Nilikimbia na kutafuta ufumbuzi ili niweze kumuokoa na namshukuru Mungu niliweza kupanda upande wa mbele wa jengo hilo mpaka kufika kwenye balkoni.

Gassama alifika mpaka ghorofa ya nne na kufikia balkoni hiyo na hatimaye kumuokoa mtoto huyo kwa kutumia mkono mmoja.

Wakati wazimamoto walipofika kwenye tukio, mtoto huyo wa miaka minne alikuwa tayari amesalimika.

"Bahati, kulikuwa na mtu aliyekuwa na nguvu na ushujaa wa kupanda na kumuokoa mtoto huyo," msemaji wa zimamoto ameiambia AFP, Shirika la habari la Ufaransa.

XS
SM
MD
LG