Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 09, 2023 Local time: 12:26

Rais wa Ukraine kukutana na Rais wa Marekani


Rais Volodymyr Zelenskiy
Rais Volodymyr Zelenskiy

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anatembelea White House kwa mazungumzo Jumatano na Rais wa Marekani, Joe Biden.

Ziara ya kiongozi huyo ambayo imekuwa ikifanyiwa kazi kwa miezi miwili na ilicheleweshwa kwa sababu ya mashauriano kuhusu matukio huko Afghanistan.

Maafisa waandamizi katika utawala wa Marekani walisema ujumbe wa ziara hiyo ni nia ya dhati ya Marekani kwa uhuru wa Ukraine, uadilifu wa kieneo na matarajio ya Euro-Atlantiki.

Maafisa hao waliwaambia waandishi wa habari, ajenda zitajumuisha masuala ya usalama, sera ya nishati na hali ya hewa, pamoja na juhudi za kupambana na ufisadi nchini Ukraine.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin (R) akishiriki katika tafrija ya kumkaribisha Rais Volodymyr Zelensky, Pentagon, Washington, DC, Agosti 31, 2021.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin (R) akishiriki katika tafrija ya kumkaribisha Rais Volodymyr Zelensky, Pentagon, Washington, DC, Agosti 31, 2021.

Maafisa hao pia walisema pande hizo mbili, zitatangaza makubaliano kadhaa pamoja na msaada wa usalama kwa Ukraine, misaada ya kibinadamu kwa wale walioathiriwa na mgogoro wa Russia huko mashariki, na misaada inayohusiana na virusi vya Corona.

XS
SM
MD
LG