Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 12:48

Wahamiaji zaidi wafa kwenye bahari ya Atlantic


Wahamiaji kutoka Afrika wakiwa kwenye visiwa vya Canary Uhispania
Wahamiaji kutoka Afrika wakiwa kwenye visiwa vya Canary Uhispania

Maafisa wa Uhispania wamesema Jumanne kwamba takriban watu 11 wanahofiwa kufa, baada ya boti nyingine kutumbukia kwenye bahari ya Atlantic ikitokea Afrika kaskazini kuelekea kwenye visiwa vya Canary nchini humo. 

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP,maafisa wa serikali ya Hispania waliotumwa kwenye visiwa vya Canary wamesema wahamiaji 32 wameokolewa wakiwa na mwili wa mmoja wao aliyekufa, karibu na kisiwa cha Fuerventura, kilichoko karibu na ufukwe wa Afrika.

Baadhi ya watu waliookolewa wamesema kwamba boti yao ilikuwa na jumla ya wahamiaji 60 ilipong’oa nanga kwenye mji wa kusini mwa Morocco wa Tan-Tan siku nne zilizopita. Shirika Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM, linasema kwamba wahamiaji 529 wamekufa mwaka huu wakati wakijaribu kuvuka bahari wakielekea kwenye visiwa vya Uhispania.

IOM limeongeza kusema kuwa huenda idadi hiyo ikawa kubwa zaidi kutokana na kuwa kuna wale ambao hutoweka kwenye bahari bila kujulikana wakati miili yao pia ikipotea. Baadhi wa wahamiaji waliookolewa katika siku za nyuma wamesema kwamba miili ya wale wanaokufa wakiwa safarini mara nyingi hurushwa baharini.

XS
SM
MD
LG