Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 12:56

Taliban washerehekea baada ya Wamarekani kuondoka Afghanistan


Sherehe mjini Kabul, Afghanistan.
Sherehe mjini Kabul, Afghanistan.

Milio ya risasi ya sherehe ilisikika kote Kabul chini Afghanistan Jumanne wakati wapiganaji wa Taliban walipodhibiti uwanja wa ndege wa Kabul kabla ya alfajiri, kufuatia kuondoka kwa wanajeshi wa mwisho wa Marekani.

Kuondoka huko kunashiria kumalizika kwa vita vya miaka 20 ambavyo viliwaacha wanamgambo wa Kiislam wakiwa na nguvu kuliko ilivyokuwa mnamo mwaka wa 2001.

Picha za video zilizosambazwa na Taliban zilionyesha wapiganaji wakiingia kenye uwanja huo wa ndege baada ya wanajeshi wa mwisho wa Marekani kuondoka kwa ndege ya C-17 dakika moja kabla ya usiku wa manane, katika kile kinachotajwa na baadhi ya wachambuzi kama kisa cha aibu kwa Washington na washirika wake wa NATO.

"Ni siku ya kihistoria na wakati wa kihistoria," msemaji wa Taliban Zabihullah Mujahid aliwaambia waandishi wa habari katika uwanja wa ndege baada ya kuondoka kwa Wamarekani.

"Tunajivunia nyakati hizi, kwamba tuliikomboa nchi yetu kutoka kwa nchi zenya nguvu kubwa," aliongeza.

Picha kutoka Pentagon ilionyesha mwanajeshi wa mwisho wa Marekani akiingia ndani ya ndege ya mwisho ya uokoaji kutoka Kabul.

Vita hivyo nchini Afghanistan ndivyo vya muda mrefu zaidi kwa Marekani, vikigharimu takriban dola trilioni mbili, na vilimalizika kwa wanamgambo wenye msimamo mkali wa Kiislam kudhibiti eneo zaidi kuliko wakati wa utawala wao uliopita.

Zaidi ya watu 123,000 wameondoka nchini humo kwa kuhofia utawala wa Taliban.

XS
SM
MD
LG