Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 30, 2022 Local time: 14:35

Marekani yaitaka Russia kuacha uchokozi dhidi ya Ukraine


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken (Kulia) na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ametoa wito kwa Rashia kukomesha hatua zake za uvamizi na uchokozi dhidi ya Ukraine, akisema kwamba Moscow imeweka idadi kubwa ya wanajeshi wake kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili.

Blinken alitoa matamshi Alhamisi alipokutana na rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine mjini Kiev, alipokuwa nchini humo kwa ziara ya siku moja na kusisitiza kwamba Marekani inasimama pamoja na nchi hiyo.

Ziara hiyo ya Blinken imefanyika kufuatia uwamuzi wa Rashia mwezi uliyopita kupeleka zaidi ya wanajeshi laki moja kwenye mpaka wake na Ukraine na kuwaondowa haraka baadae.

Rais Zelensky amesema wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi Habari kwamba licha ya kuondolewa kwa wanajeshi wa Rashia, nchi yake ingali inakabiliwa na kitisho kutoka Rashia.

Kabla ya kukutana na rais wa Ukraine, mwanadiplomasia mkuu wa Marekani alikua na mazungumzo na waziri mwenzake Dmytro Kuleba na kusisitiza kwamba Washington inataka kufanya kazi na Kiev kuimarisha juhudi zake za usalama pamoja na kuleta demokrasia ya kweli na kupambana na ulaji rushwa.

Kwa kuitembelea Ukraine mapema kabla ya Rashia, Blinken anatoa ishara kwamba Ukraine iko juu kwenye ajenda ya mambo ya kigeni ya utawala wa Biden.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG