Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 12, 2024 Local time: 02:29

Upinzani Russia waitisha maandamano kuokoa maisha ya Navalny


Alexei Navalny
Alexei Navalny

Washauri wa kiongozi wa upinzani wa Rashia anaeugua jela Alexei Navalny akiwa katijka wiki ya tatu ya mgomo wa chakula, wametoa wito kwa warashia kuandamana siku ya Jumatano ili kuokoa maisha yake.

Mshauri wake Leonid Volkov ameandika kwenye ukurasa wa Facebook kwamba huu ndio wakati wa kuchukua hatua akiongeza kusema hawahitajiki kuzungumzia uhuru wa Navalny pekee bali, maisha yake pia.

Volkov amesema maandamanio ya Jumatano yanaweza kuwa vita vikuu dhidi ya ukatili au maandamano makubwa ya upinzani kwa miaka kadhaa ijayo.

Wito huo umetolewa siku moja baada ya daktari wake, Yaroslav Ashikhmin kuonya kwamba afya ya kiongozi huyo wa upinzani mwenye umri wa miaka 44 inaendelea kuwa mbaya kwa haraka na huenda akafariki ghafla kutokana na matatizo ya figo.

Navlany mkosoaji mkuu wa Rais wa Rashia Vladimir Putin alianza mgomo wa kutokula Machi 31 akidai kupewa matibabu anayostahiki kwa maumivu ya mgongo na kufaganzi kwa migu na mikono.

XS
SM
MD
LG