Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 30, 2023 Local time: 14:46

Mwanaharakati wa Russia awasili Ujerumani kwa matibabu


Alexei Navalny

Mwanasiasa mashuhuri wa upinzani wa Russia Alexei Navalny ambaye yuko mahututi baada ya tuhuma za kuwa alipewa sumu, amewasili katika mji mkuu wa Ujerumani, Berlin, Jumamosi asubuhi kwa ndege maalum, ambako atapatiwa matibabu katika hospitali kuu mjini hapo.

Madaktari wa Russia walitangaza hapo awali kwamba wamekubaliana na maombi kumruhusu Navalny kupatiwa matibabu Ujerumani – na hivyo kumaliza mzozo juu ya nani atamuangalia mwanasiasa huyo kufuatia kile ambacho familia ya Navanly imesema ilikuwa ni jaribio la makusudi la kumua alipokuwa anatembelea Siberia mapema wiki hii.

Dkt Anatoly Kalinichenko wa Hospitali No. 1 katika mji wa Omsk, Russia akizungmza na waandishi wa havari.
Dkt Anatoly Kalinichenko wa Hospitali No. 1 katika mji wa Omsk, Russia akizungmza na waandishi wa havari.

Kabla ya kusafirishwa Ijumaa Dkt Anatoly Kalinichenko wa Hospitali No. 1 katika mji wa Omsk, ambako Navalny alikuwa hana fahamu na amewekewa kifaa cha kumsaidia kupumua amesema “Hali ya mgonjwa inaendelea kuimarika.”

Ameongeza kusema kwamba, “wakati tumepokea ombi la wanafamilia kumruhusu mgonjwa kusafirishwa, hivi sasa tumefikia uamuzi hatuna pingamizi kusafirishwa kwake kwenda kutibiwa hospitali nyingine.”

Kalinichenko pia amesema kuwa “baada ya kupokea ombi la wanafamilia juu ya kusafirishwa kwa mgonjwa,” familia ya Navalny itasimamia kikamilifu jukumu la safari hiyo.”

Uamuzi huo umefikiwa katika siku iliyokuwa ina mvutano wakati madaktari wa Russia hapo awali walikata shauri kuwa ni hatari kabisa kumsafirisha Navalny lakini baadae walibadilisa mawazo baada ya shinikizo la umma lililopigia kelele jambo hilo.

Hilo limetokea baada ya mke wa Navalny, Yulia Navalnaya kutoa tamko hadharani akimuomba Rais wa Russia Vladimir Putin, kupitia mtandaoni, kusaidia juu ya suala hilo.

Wafuasi wa Navalny pia walijadili kuwa kuchelewesha kwa namna yoyote ile kupelekwa kufanyiwa matibabu yatayaweka maisha ya mwanasiasa huyo hatarini – na , pengine itazuia kugundua kitu gani kilimuathiri kwa ghafla mwanasiasa huyo.

Ndege iliyokodishwa na shirika la misaada ya kibinadamu ya Ujerumani ikiwa na historia ya kuwasaidia kwa siri wapinzani wa kisiasa kutoka Russia, Cinema for Peace, iliwasili Omsk mapema Ijumaa.

Madaktari waliokuwa wamewasili na ndege hiyo walikuwa wanaamini Navalny alikuwa katika hali inayoruhusu kusafirishwa, saa kadhaa kabla ya Madaktari wa Russia kutoa tathmini ya mgonjwa inayolingana na ile ya madaktari wa Ujerumani.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG