Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 05, 2022 Local time: 13:45

Baraza la Kijeshi Mali kutangaza serikali ya mpito karibuni


Wanajeshi wakifanya doria katika mitaa ya Bamako, Mali, Aug. 19, 2020.

Baadhi ya vyama vya siasa vya Mali vimelaani mapinduzi ya kijeshi yaliofanyika mapema wiki hii na kutaka kuundwa kwa haraka utawala wa mpito wa kiraia.

Lakini viongozi wa vyama vya upinzani na vuguvugu la kutaka mageuzi nchini humo la M5-RFP wanaunga mkono msimamo wa Baraza la Kijeshi CNSP, na kupongeza mapinduzi hayo, huku wakiitaka Jumuia ya uchumi ya Afrika Magharibi, ECOWAS, kutoingilia kati masuala ya ndani ya nchi yao.

Wakati huo huo ECOWAS imetangaza kwamba inapeleka ujumbe viongozi mjini Bamako ili kuwataka wanajeshi kurudisha mara moja utawala wa kikatiba na kiraia na kumuachilia huru Rais Ibrahimi Boubacar Keita na maafisa wa serikali yake.

Meja Knali Ismael Wague, kati kati, msemaji wa Baraza la kijeshi CNSP
Meja Knali Ismael Wague, kati kati, msemaji wa Baraza la kijeshi CNSP

Baraza jipya la utawala wa kijeshi nchini Mali CNSP linapinga uingiliaji kati wa nchi za kigeni katika masuala ya ndani ya nchi hiyo na limetangaza Alhamisi kwamba litaunda serikali ya mpito hivi karibuni baada ya kukutana na viongozi wa vyama vyote vya kisiasa na asasi za kiraia.

Mwenyekiti wa kamati ya utendaji ya M5-RFP Choguel Maiga amewaonya wale walioiwekea nchi yake vikwazo kwamba wanakiuka makubaliano ya kimataifa.

Choguel Maiga, mwenyekiti wa kamati ya utendaji ya M5-RFP: "Ikiwa rais wa zamani Ibrahim Boubacar Keita alitangaza kujiuzulu na kuivunja serikali na bunge na jumuia ya kimataifa imeshuhudia, tunajiuliza inawahusu nini ECOWAS kuingilia kati."

Matamshi hayo yametolewa baada ya Viongozi wa ECOWAS kukutana kwa kikao cha dharura Alhamisi kupitia mtandao na kuamua kwamba wanapeleka ujumbe wa viongozi wa juu . Rais wa Niger Mahamadou Issoufu ambae ni mwenyekiti wa ECOWAS hivi sasa, anasema wakati wa mapinduzi umekwisha.

Mahamadou Issoufou, Rais wa Niger, Mwenyekiti wa ECOWAS: "Kwa hivyo tutaanza majadiliano na viongozi wa baraza la kijeshi ili kuwasilisha ujumbe wa jumuiya yetu na kuwafahamisha kwamba muda wa kuchukua madaraka kwa nguvu umekwisha."

Rais Issoufou Mahamadou wa Niger, Mwenyekiti wa ECOWAS
Rais Issoufou Mahamadou wa Niger, Mwenyekiti wa ECOWAS

Viongozi wa ECOWAS wametoa wito wa kuachiliwa kwa Rais Keita na maafisa wake na kurudishwa madarakani mara moja kulingana na katiba ya Mali.

Msimamo huo unaungwa mkono na vyama kadhaa vya kisiasa nchini Mali ambavyo vinasema vinalaani mapinduzi lakini hivi sasa yamefanyika hivyo inabidi mazungumzo kuanza ili kuunda utawala wa mpito kuelekea uchaguzi mpya.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG