Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 24, 2023 Local time: 17:58

Putin asaini sheria kusalia madarakani hadi mwaka 2036. Marais wa zamani kutofunguliwa mashtaka


Rais wa Russia Vladmir Putin

Rais wa Russia Vladmir Putin amesaini sheria inayotoa kinga ya kutoshitakiwa kwa waliokuwa marais wa nchi hiyo.

Sheria hiyo vile vile inatoa fursa kwa marais wa zamani kuwa maseneta wa maisha katika bunge la juu la nchi hiyo, punde tu wanapoondoka madarakani.

Sheria hiyo inafuatia mabadiliko makubwa ya kisiasa ambayo yamefanywa na Putin nchini Russia, mwaka huu.

Sheria hiyo ni sehemu ya mabadiliko ya katiba yaliyopitishwa kote nchini humo mwaka huu, na kumruhusu Putin kusalia madarakani hadi mwaka 2036.

Alikuwa anatarajiwa kuondoka madarakani mwaka 2024.

Marais wa Zamani wa Russia walikuwa tayari na kinga ya kisheria, kutoshitakiwa kutokana na makosa waliofanya walipokuwa madarakani.

Sheria ya sasa inatoa kinga ya kutoshitakiwa maisha yao yote, hawawezi kukamatwa, kukaguliwa, kuchunguzwa wala kufunguliwa mashtaka.

Sheria mpya pia inaweka mazingira magumu kabisa ya kuondoa kinga ya kutoshitakiwa kwa marais wa zamani.

XS
SM
MD
LG