Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 31, 2024 Local time: 01:01

Fauci atahadharisha kutokea maambukizi hadi milioni 1 Marekani


Dkt Anthony Fauci
Dkt Anthony Fauci

Mtaalam wa juu wa magonjwa ya kuambukiza nchini Marekani alikiambi kituo cha televisheni cha CNN Jumapili kwamba kunaweza kuwa na vifo hadi milioni 1 vya COVID-19 nchini Marekani ifikapo mwishoni mwa mwaka, lakini hali wakati inatabirika kabisa pia inazuilika.

Dkt Anthony Fauci alisema Marekani ina njia za kuepuka kutokea kwa utabiri huu, lakini shida ni watu milioni 80 nchini ambao hawajachanjwa.

“Tunaweza kugeuza jambo hili na tunaweza kulifanya kwa ufanisi na haraka ikiwa tunaweza kuwapa watu hao chanjo," Fauci alisema.

"Ni muhimu sana kwamba watu katika mzozo huu kuweka kando tofauti zozote za kiitikadi na kisiasa na kupata chanjo “ aliongeza.

Wakati huo huo, wiki iliyopita, Marekani ilifikia wastani wa kila siku wa kulazwa kwa watu laki 1 kutokana na COVID-19, kulingana na ripoti ya New York Times.

Ripoti hiyo ilisema kuongezeka huko kwa maambukizi kunashindana tu na kuongezeka kwa msimu wa baridi uliopita wakati chanjo hazikuwepo.

XS
SM
MD
LG