Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 02, 2024 Local time: 00:54

Marekani yaonya raia wake kutokwenda Uingereza kwasababu ya ongezeko la maambukizi ya Covid 19


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken alipozungumza na viongozi wa Chile.July 16, 2021 (Tom Brenner/Pool via AP)
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken alipozungumza na viongozi wa Chile.July 16, 2021 (Tom Brenner/Pool via AP)

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani inawasihi  Wamarekani kutosafiri kwenda Uingereza kwa sababu ya kuongezeka kwa visa vipya vya COVID-19 nchini humo

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani inawasihi Wamarekani kutosafiri kwenda Uingereza kwa sababu ya kuongezeka kwa visa vipya vya COVID-19 nchini humo.

Wizara hiyo iliweka tahadhari ya usafiri kwenda Uingereza kwa kiwango cha juu Jumatatu, kufuatia hatua kama hiyo iliyochukuliwa na Vituo vya Udhibiti na Kuzuia Magonjwa vya Amerika mapema siku hiyo.

Taasisi zote mbili zilisema ikiwa ni lazima watu wasafiri kwenda Uingereza wahakikishe kuwa wamepewa chanjo zote kamili kabla ya safari yao

Ushauri huo uliofanyiwa marekebisho ulitolewa wakati watu wa Uingereza walisherehekea kile kilichoitwa "Siku ya Uhuru," ikiwa ni kuadhimisha mwisho rasmi wa karibu vizuizi vyote vya kufunga shughuli za kiuchumi pamoja na uvaaji wa lazima wa barakoa na umbali wa kijamii.

XS
SM
MD
LG