Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 03, 2024 Local time: 08:45

Biden asisitiza Marekani itasimama na washirika wake dhidi ya Russia


File : Mnamo Machi 10, 2011, Makamu wa Rais Joe Biden, kushoto, akipeana mkono na Waziri Mkuu wa Russia Vladimir Putin in Moscow, Russia. (RIA Novosti, Alexei Druzhinin/Pool via AP, file)
File : Mnamo Machi 10, 2011, Makamu wa Rais Joe Biden, kushoto, akipeana mkono na Waziri Mkuu wa Russia Vladimir Putin in Moscow, Russia. (RIA Novosti, Alexei Druzhinin/Pool via AP, file)

Rais wa Marekani Joe Biden amesema nchi yake itasimama imara na washirika wake wa Ulaya dhidi ya Russia, kuelekea kwa mkutano wa kwanza wa ana kwa ana na rais Vladimir Putin.

Biden atakwenda Ulaya Jumatano na amepanga kuhudhuria mkutano wa nchi saba zenye uchumi mkubwa duniani, G-7, na ushirika wa kijeshi wa NATO, na baadaye kukutana na kiongozi wa Russia mjini Geneva, Uswizi, tarehe 16 mwezi huu.

Mkutano huo unafanyika huku mgogoro mkubwa katika uhusiano baina ya nchi hizo mbili ukiendelea kwa miaka mingi, na mivutano kuhusu masuala kadhaa ikiwa ni pamoja na Marekani kuishutumu Russia kwa udukuzi wa kimitandao, uingiliaji wa uchaguzi na ukiukaji wa haki za binadamu.

Katika waraka uliochapishwa na gazeti la Washington Post Jumamosi, Biden ameahidi kuunga mkono kile anachokiita "ushirikiano wa kidemokrasia" wa Washington, wakati wa mizozo na vitisho vingi kutoka Moscow na Beijing.

"Tunasimama kidete kushughulikia changamoto za Russia kwa usalama wa Ulaya, tukianza na uchokozi wake huko Ukraine, na hakutakuwa na shaka juu ya azma ya Marekani kutetea maadili yetu ya kidemokrasia, ambayo hatuwezi kuyatenga na masilahi yetu," aliandika.

Tangu aingie madarakani Januari mwaka 2021, Biden ameongeza shinikizo kwa Kremlin, na maoni yake yaliyomfananisha Putin na "muuaji" yalikosolewa vikali na Moscow.

XS
SM
MD
LG