Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 07, 2024 Local time: 11:12

Utawala Rais Biden unaanzisha rasmi vita dhidi ya ufisadi


Rais Joe Biden akishuka kwenye ndege ya Air Force One Maryland Juni 1, 2021. MANDEL NGAN / AFP
Rais Joe Biden akishuka kwenye ndege ya Air Force One Maryland Juni 1, 2021. MANDEL NGAN / AFP

Utawala wa Rais wa Marekani Joe Biden unaanzisha rasmi vita dhidi ya ufisadi kama msingi wa usalama wa kitaifa.

Biden siku ya Alhamisi alitoa risala yake ya kwanza ya usalama wa kitaifa, akielezea ajenda yake ya kupambana na ufisadi.

Rushwa inatishia usalama wa kitaifa wa Marekani, usawa wa uchumi, juhudi za kupambana na umaskini ulimwenguni na juhudi za maendeleo. Na demokrasia yenyewe, rais alisema katika maagizo yake. "Lakini kwa kuzuia kikamilifu na kupinga ufisadi na kuonyesha faida za utawala wa uwazi na uwajibikaji, tunaweza kupata faida muhimu kwa Marekani na demokrasia nyingine." alisema Biden.

Waraka wa Biden unatumika kama taarifa rasmi kutoka kwa rais kwamba anatarajia idara na mashirika yote ya serikali kuu kuendeleza shughuli zao za kupambana na ufisadi kwa njia ya kipekee kabisa, afisa mwandamizi wa utawala aliwaambia waandishi wa habari kwa njia ya simu Alhamisi

XS
SM
MD
LG