Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 11:03

Rais Biden ashiriki kumbukumbu ya maadhimisho ya miaka 100 ya mauaji ya Tulsa


Rais wa Marekani Joe Biden akizungumza katika maadhimisho ya miaka 100 ya mauaji ya Tulsa katika kituo cha Greenwood mjini Tulsa, Oklahoma, June 1, 2021.
Rais wa Marekani Joe Biden akizungumza katika maadhimisho ya miaka 100 ya mauaji ya Tulsa katika kituo cha Greenwood mjini Tulsa, Oklahoma, June 1, 2021.

Rais wa Marekani Joe Biden amekuwa rais wa kwanza aliyeko madarakani kwenda Tulsa, Oklahoma kuadhimisha kumbukumbu miaka mia moja ya Mauaji ya Tulsa, pale kikundi cha wazungu walipofanya waharibifu mwaka 1921 kwa jamii ya Weusi ambapo watu 300 walikufa na 10,000 wakiachwa bila makazi.

Biden alitembelea Kituo cha Utamaduni cha Greenwood na kutoa hotuba huko kuadhimisha miaka 100.

Kwa vile historia imekuwa kimya, haina maana kwamba hayo hayakufanyika, Biden alisema katika matamshi yake kwa manusura wa mauaji hayo na familia zao katika kituo cha utamaduni cha Greenwood. Baadhi ya ukosefu wa haki ulikuwa ni wa kinyama, wa kutisha, mbaya sana, hauwezi kufichwa, bila ya kujali watu wanajaribu kwa nguvu kiasi gani.

Miaka 100 iliyopita mnamo May 31 na Juni 1, Greenwood, eneo lililokuwa likijulikana kama Black Wall Street, ulikumbwa na wizi wa ngawira na kuchomwa kwa majengo vitendo ambavyo vilifanya na wakazi wazungu ambao walikuwa wakiungwa mkono na polisi weupe wa huko Tulsa.

Mauaji hayo yalichochewa na shutuma kwamba kijana mweusi mwenye umri wa miaka 19 alimshambulia msichana wa kizungu mwenye umri wa miaka 17 katika lifti.

XS
SM
MD
LG