Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 13:36

Serikali yasitisha huduma za Twitter Nigeria


Rais Muhammadu Buhari (Twitter/ @BashirAhmaad)
Rais Muhammadu Buhari (Twitter/ @BashirAhmaad)

Makampuni ya mawasiliano ya simu ya Nigeria yamesitisha huduma za mtandao wa kijamii wa Twitter nchini humo Jumamosi, kufuatia maagizo ya serikali.

Maamuzi hayo yamelenga kusimamisha kwa muda usiojulikana, huduma za kampuni hiyo kubwa ya Marekani, hatua iliyokosolewa na watetezi wa haki, na wanadiplomasia, kama kuminya uhuru wa kujieleza, imeripoti Reuters.

Serikali ya Nigeria ilisema Ijumaa ilikuwa imesimamisha shughuli za Twitter kwa muda usiojulikana, siku mbili baada ya mtandao huo kuondoa tweet ya Rais Muhammadu Buhari, ambayo ilitishia kuwaadhibu watu wanaounga mkono mfumo wa kujitenga kwa baadhi ya majimbo nchini humo.

Kampuni ya Twitter, ambayo haikupatikana mara moja kutoa maoni leo Jumamosi, ilisema hapo jana kwamba ilikuwa ikichunguza kusimamishwa huko, ambako ilisema kunatia wasiwasi mkubwa.

Twitter logo
Twitter logo

Serikali ya Buhari, ambayo inasimamia uchumi mkubwa zaidi barani Afrika, mwaka jana ilipendekeza sheria ya kudhibiti mitandao ya kijamii, kufuatia maandamano dhidi ya madai ya ukatili wa polisi.

Kundi la kutetea haki la Amnesty International lililaani kusimamishwa kwa shughuli za Twitter, na limewataka viongozi wa Nigeria "kubatilisha msimamo wao na kusitisha mipango mingine ya kuzuia vyombo vya habari, kukandamiza haki za raia, na kudhoofisha haki za binadamu za wanijeria."

XS
SM
MD
LG