Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Agosti 17, 2022 Local time: 13:21

Wanamgambo wauwa wanajeshi 30 Nigeria


Wanamgambo wenye msimamo mkali wameuwa wanajeshi 30 wa serekali katika mfululizo wa mapigano kaskazini mashariki mwa Nigeria toka Jumatano, kwa mujibu vyanzo vya kijeshi na raia.

Shirika la habari la Reuters linaeleza kwamba usalama kote Nigeria, umezorota katika miezi ya hivi karibuni ikijumuisha kaskazini mashariki.

Mashambulizi manne yamesababisha vifo vya wanajeshi 27, na wanamgambo wa kikosi cha raia 10, ikijumuisha mkuu wa kikosi, kwa mujibu wa chanzo cha Reuters.

Jeshi na msemaji wa wizara ya ulinzi hawakuwa tayari kujibu simu na ujumbe uliopelekwa ili kutoa ufafanuzi wa habari za mashambulizi hayo.

Kundi la Islamic State West Province (ISWAP), ambalo lina ushirikiano na kundi la Islamic State, limedai kuhusika na mashambulizi ya Ijumaa ya Monguno, kupitia shirika la habari la Amaq siku ya Jumamosi.

ISWAP limedai kuua wanajeshi 33 na kumkamata mmoja.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG