Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 04:41

Nigeria : Boko Haram ni pingamizi la wakazi kurejea maeneo waliokimbia


Wanawake wamekusanyika katika kambi ya El-Miskin Agosti 20, 2020 mji wa Maiduguri.
Wanawake wamekusanyika katika kambi ya El-Miskin Agosti 20, 2020 mji wa Maiduguri.

Wanamgambo wa Boko Haram wamewatishia usalama wakazi wa eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria kwa zaidi ya muongo mmoja, na kupelekea zaidi ya watu milioni 2 kukimbia makazi yao, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Watu wasiopungua 3,000 wamekimbia kutoka maeneo ya ndani mwa nchi na kuishi katika maeneo yaliyo na usalama kiasi ya Kawar Maila, kambi moja iliyoko mji mkuu wa Jimbo la Borno, Maiduguri.

Ilivyokuwa wamekimbia kikundi cha Kiislamu chenye msimamo mkali, watu hawa waasiokuwa na makazi bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali, kutafuta chakula na huduma za msingi za afya, kuelimisha watoto wao, huku wakitafakari mustakbali uliobora.

“Maisha hapa ni magumu sana. Tunapata tabu,” amesema Mohammed Abba, ambaye alikuwa na shamba katika eneo la serikali la Konduga, kiasi cha kilomita 25 kusini mashariki mwa Maiduguri. Hivi sasa, yeye, na mkewe na watoto watano wanaishi katika chumba kimoja kwa kubanana.

FILE - Watu waliokimbia makazi yao kutokana na tishio la Boko Haram wakisubiri kuchota maji katika kambi ya Muna Maiduguri, Nigeria, Aug. 30, 2016.
FILE - Watu waliokimbia makazi yao kutokana na tishio la Boko Haram wakisubiri kuchota maji katika kambi ya Muna Maiduguri, Nigeria, Aug. 30, 2016.

“Wakati wa msimu wa mvua, utashtuka kuona vipi tunalazimika kukabiliana na maisha hayo. Chumba hiki kinajaa maji na hatuwezi kulala humu ndani,” amesema. Abba alikuwa anafuga wanyama na kufanya biashara. Lakini hii ndio hali yetu hivi leo.

Jirani yake Falmata Abukar pia ametokea Konduga na mumewe. Analaumu kile anachofikiria kutokuwepo huduma za afya inayokidhi mahitaji katika kambi kukabiliana na hali ya mtoto wake wakiume ambaye jicho lake moja linapofuka taratibu.

“Mwanangu aliugua. Alikuwa hajafungua macho yake kwa siku nne. Hawezi hivi sasa kuona kwa jicho hilo,” Abukar amesema. “Jicho hilo haliwezi kuokolewa.”

Wajane, wengi wao wakiwa na watoto, wanaishi katika ghala iliyotolewa msaada – zaidi ya watu 180 wamepewa vyumba vilivyo tenganishwa kwa vitambaa au plastiki. Wanawake mara nyingi wanakaa pamoja katika kituo hicho, wakizungumza huku wakichambua mahindi ili kutengeneza chakula cha asili kinachoitwa bisko.

Wakazi wa kambi hiyo, wamezuiliwa kuendelea na shughuli zao za kawaida, wanajaribu kujikimu kimaisha. Wakati wa mchana wakiwa nje, wanawake wanajishughulisha na ushonaji, utengenezaji kofia na vitu vingine vya kuuza. Hivyo hivyo wasichana wanajishughulisha na kazi hizo ambapo wangekuwa shule iwapo wangekuwepo katika jamii zao kwenye makazi walioyakimbia.

XS
SM
MD
LG