Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 23:47

Boko Haram washambulia vijiji kadhaa Nigeria na kufanya mauaji


Kundi la wapiganaji la Boko Haram limeaua watu 10 wakiwemo maafisa wanne wa usalama baada ya kushambulia vijiji vitatu kaskazini mwa Nigeria.

Wapiganaji hao wamevamia vijiji vya Shafa, Azare na Tashan Alade katika jimbo la Borno, na kuchoma moto nyumba kadhaa zikiwemo ofisi za serikali kabla ya kufyatua risasi kiholela dhidi ya wakaazi wa vijiji hivyo.

Wapiganaji hao walishambulia Kijiji baada ya kingine.

Katika Kijiji cha Azare, walichoma moto kituo cha polisi na kuua maafisa wawili wa polisi, mwanajeshi na afisa wa ujasusi.

Wakaazi wa vijiji hivyo walitorokea msituni kufuatia mashambulizi hayo.

Kundi la Boko Haram limeongeza mshambulizi dhidi ya raia katika siku za hivi karibuni.

Kundi hilo limedai kuhusika na shambulizi lililoua watu 11 na kuteka nyara watu mkesha wa krisimasi.

Kulingana na umoja wa mataifa, kundi la Boko Haram limeua zaidi ya watu 36,000 kaskazini mashariki mwa Uganda na kusababisha karibu watu milioni 2 kutoroka makwao tangu mwaka 2009.

XS
SM
MD
LG