Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 29, 2023 Local time: 08:26

Prof Abdulrazak mwenye asili ya Tanzania ashinda tuzo ya Fasihi ya Nobel


Mshindi wa Tuzo ya Fasihi ya Nobel Abdulrazak Gurnah akiwa nyumbani kwake Canterbury, Uingereza, Oct. 7, 2021.

Mwandishi wa riwaya, mzaliwa wa Tanzania, Abdulrazak Gurnah Alhamisi ameshinda tuzo ya Fasihi ya Nobel. 

Gurnah, aliyekulia visiwani Zanzibar na kuhamia nchini Uingereza kama mkimbizi katika kipindi cha mwisho cha miaka ya 1960, ni Muafrika wa tano kushinda tuzo ya Fasihi ya Nobel.

Taasisi ya Sweden imesema Gurnah amepewa tuzo hiyo “kwa udadisi na shauku yake ya kuangalia kwa kina athari za ukoloni na hatma ya wakimbizi katika mwanya uliopo kati ya tamaduni mbalimbali na mabara mbalimbali.”

“Vitabu vyake vya riwaya vinaanzia kwenye maelezo ya unyanyapaa na inafungua maono yetu katika utamaduni pana za Afrika Mashariki ambazo hazijulikani na wengi katika maeneo mengine ya dunia,” taasisi ya Nobel imeeleza.

Gurnah ameiambia tovuti ya Nobel Prize alishtushwa kupokea simu kutoka kwa Taasisi ya Sweden.

Ameachapisha vitabu 10 na hadithi fupifupi kadhaa.

Baadhi ya vitabu vya mwandishi wa riwaya Abdulrazak Gurnah
Baadhi ya vitabu vya mwandishi wa riwaya Abdulrazak Gurnah

Mkuu wa kamati ya tuzo za Nobel, Anders Olsson, amesema mitizamo ya Gurnah kwa matatizo ya wakimbizi ni yenye kuendana na wakati.
"His writings are extremely interesting right now for many, many people in Europe and around the world," Olsson told reporters.

“Vitabu vyake hivi sasa vina mvuto zaidi kwa wengi, wengi wa watu wa Ulaya na duniani kote,” Olsson aliwaambia waandishi.

Baada ya kushinda tuzo hiyo, Gurnah amewataka watu wa Ulaya kuwaangalia wakimbizi wa Afrika kama ni rasilimali, akisema kuwa “wengi wa watu hawa wanaokuja huku Ulaya, wanakuja kutokana na shida, na pia kwa kweli wanacho kitu cha kuwapa.”

“Hawaji mikono mitupu. Wengi wanavipaji, ni watu wenye hamasa wanacho kitu cha kutoa kwa wengine,” Gurnah ameiambia taasisi ya Nobel katika mahojiano.

Tangazo la ushindi wake limekuja kwa mchapishaji wa Sweden wa vitabu vya Gurnah bila matarajio.

Inawezekana nimesikia mtu akikadiria mara moja kuwa vitabu vyake vinahadhi ya Nobel. Lakini sikutarajia yeye kupata tuzo hiyo,” Henrik Celander ameliambia shirika la habari la Sweden TT.

Gurnah alizaliwa mwaka 1948, na akuondoka Zanzibar mwaka 1968 kufuatia mapinduzi yaliyopelekea ukandamizaji na kufunguliwa mashtaka kwa raia wenye asili ya Kiarabu.

Alianza kuandika akiwa na umri wa miaka 21 nchini Uingereza. Pamoja na kuwa Kiswahili ilikuwa ndio lugha yake ya kwanza, Kiingereza kikawa ni nyenzo yake ya uandishi.

Gurnah ni mashuhuri kwa kitabu chake kilichotoka mwaka 1994 maarufu “Paradise”, kikieleza ukoloni huko Afrika Mashariki wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia kiliorodheshwa katika Tuzo ya Booker Prize for Fiction.

Kitabu hicho bila shaka kinanukuu kutoka kitabu maarufu cha mwaka 1902 cha mwandishi wa Uingereza Joseph Conrad “Heart of Darkness” kinachoeleza safari ya shujaa kijana mwaminifu Yusuf kuelekea Afrika ya Kati na Bonde la Congo.

Vitabu vya mwandishi wa riwaya katika maonyesho huko Sweden.
Vitabu vya mwandishi wa riwaya katika maonyesho huko Sweden.

Gurnah has until his recent retirement been Professor of English and Postcolonial Literatures at the University of Kent in Canterbury, focusing principally on writers such as Wole Soyinka, Ngugi wa Thiong'o and Salman Rushdie.

Gurnah hadi alipostaafu hivi karibuni alikuwa akifundisha Kiingereza na Fasihi ya kipindi baada ukoloni katika Chuo Kikuu cha Kent, Canterbury, akijikita kwa waandishi kama Wole Soyinka, Ngugi wa Thiong’o na Salman Rushdie.

Tuzo hiyo ya Nobel inakuja na medali na pesa iasi cha dola milioni 1.1.
Last year, the award went to US poet Louise Gluck.

Mwaka jana, tuzo hiyo ilikwenda kwa mshairi wa Marekani Louise Gluck.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG