Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 03:51

Chanjo ya kwanza ya Malaria kutumika Afrika


Mtoto afanyiwa majaribio ya chanjo ya Malaria kwenye picha ya awali magharibi mwa Kenya.
Mtoto afanyiwa majaribio ya chanjo ya Malaria kwenye picha ya awali magharibi mwa Kenya.

Shirika la afya duniani, WHO,Jumatano limesema chanjo ya kwanza dhidi ya Malaria iliyoidhinishwa ingepewa zaidi watoto wa Afrika,ikiwa hatua muhimu katika kupambana na ugonjwa huo ambao unaua maelfu ya watu kila mwaka.

WHO imependekeza chanjo iitwayo RTSS au Mosquirix ambayo imetengenezwa na kampuni ya dawa ya Uingereza ya GlaxoSmithKline.

Tangu mwaka wa 2019, dozi millioni 2.3 za chanjo ya Mosquirix zilitolewa kwa watoto nchini Ghana, Kenya, Malawi katika mpango kabambe unaoratibiwa na WHO.

Malaria inaua zaidi watoto walio na umri wa miaka mitano. Mpango huo uliwezekana baada ya muongo mmoja wa majaribio ya kimatibabu katika nchi saba za Afrika.

“Hii ni chanjo iliyotengenezwa Afrika na wanasayansi wa Afrika na tunajivunia sana kwa hilo hilo”, amesema mkurugenzi mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus.

Ameongeza kuwa “ kutumia chanjo hiyo pamoja na njia nyingine zilizopo za kuzuia malaria inaweza kuokoa maisha ya maelfu ya vijana kila mwaka”, akigusia hatua nyingine za kupambana na malaria kama vile vyandarua na dawa za kunyunyuzia.

Malaria inaua zaidi kuliko Covid 19 barani Afrika. Mwaka wa 2019 kulingana na makadirio ya WHO, iliua waafrika laki 3 na elfu 86 ikilinganishwa na vifo laki 2 na elfu 12 vilivyothibitishwa kutokana na Covid 19 katika miezi 18 iliyopita.

WHO inasema asilimia 94 ya visa vya malaria na vifo vinatokea Afrika, bara lenye watu billioni 1.3.

XS
SM
MD
LG