Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 26, 2022 Local time: 11:55

Serikali ya kijeshi ya Guinea yateuwa waziri mkuu.


Kiongozi wa kijeshi wa Guinea Mamadi Doumbouya wakati alipoapishwa kama rais wa mpito huko Conakry, Guinea Oktoba. 1, 2021.

Utawala wa kijeshi wa Guinea siku ya Jumatano ulimtaja Mohamed Beavogui, mfanyakazi wa zamani wa serikali na mtaalam wa fedha za kilimo, kama waziri mkuu

Utawala wa kijeshi wa Guinea siku ya Jumatano ulimtaja Mohamed Beavogui, mfanyakazi wa zamani wa serikali na mtaalam wa fedha za kilimo, kama waziri mkuu kusimamia mabadiliko yaliyoahidiwa kurejea kwenye utawala wa kidemokrasia kufuatia mapinduzi ya mwezi Septemba.

Beavogui, mwenye umri wa miaka 68, pia ni mpwa wa Diallo Telli, mwanadiplomasia maarufu wa Guinea ambaye aliwahi kuwa katibu mkuu wa kwanza wa OAU kabla ya kuundwa kwa Umoja wa Afrika, aliuwawa na utawala wa dikteta Sekou Touré mwaka 1977 .

Beavogui, ambaye uteuzi wake ulitangazwa katika amri iliyosomwa kwenye televisheni ya taifa, atasimamia mpito ambao mpango wake bado haujafafanuliwa.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG