Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 29, 2023 Local time: 08:49

Hong Kong yaelekeza nguvu zake kuvikandamiza vikundi vya kijamii


Mtendaji Mkuu wa Hong Kong Carrie Lam aonekana katika televisheni akiwasilisha hotuba ya sera ya mwaka katika Baraza la Wawakilishi Hong Kong, China Octoba 6, 2021. REUTERS/Lam Yik.

Baada ya ukandamizaji mkali dhidi ya upinzani unaounga mkono demokrasia huko Hong Kong ambao umepelekea wanaharakati kadhaa kukamatwa na kutiwa gerezani, mamlaka imeelekeza nguvu zao kwa vikundi vya kijamii vya jiji hilo.

Katika miezi ya karibuni, vikundi kadhaa maarufu vya upinzani vya Hong Kong vimegawanyika wakati hatua za ukandamizaji zikiongezeka katika jiji hilo.

Kufuatia maandamano ya mwaka 2019 dhidi ya serikali, Beijing ilitekeleza sheria ya usalama wa kitaifa.

Sheria hiyo inazuia vitendo kama kujitenga, kupindua na kushirikiana na vikosi vya kigeni.

Harakati za kidemokrasia za Hong Kong zimekwama wakati maandamano ya barabarani yamekomeshwa na hotuba za kisiasa ambazo Beijing inaona kuwa ni kama matusi zimepigwa marufuku.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG