Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 29, 2022 Local time: 17:36

Mmiliki wa vyombo vya habari Hong Kong Jimmy Lai afungwa miezi 12


Jimmy Lai

Tajiri mmiliki wa vyombo vya habari huko Hong Kong, Jimmy Lai mwenye umri wa miaka 73 amehukumiwa kifungo cha miezi 12 jela Ijumaa.

Pia katika mahakama hiyo wanaharakati wakongwe wanne wa kutetea demokrasia wamehukumiwa vifungo kati ya miezi minane hadi 18 jela.

Hukumu hiyo imetolewa kwa sababu ya watu hao kusaidia kuongoza mojawapo ya maandamano makubwa kuwahi kufanyika kwenye jiji hilo.

Lai alikuwa miongoni mwa watetezi tisa mashuhuri wa demokrasia wa Hong Kong waliopatikana na hatia ya kutayarisha na kushiriki kwenye maandamano hayo.

Wengi wao wamekuwa kwa miongo kadhaa wakitetea upigaji kura wa moja kwa moja bila ya utumiaji nguvu.

Watayariushaji wa maandamanio hayo makubwa wanasema karibu watu milioni moja laki saba walishiriki, kwenye maandamano hayo yaliyo sababisha maandamano ya miezi kadhaa huko Hong Kong mwaka 2019.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG