Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 05, 2022 Local time: 14:23

Trump kuendelea kuwawekea vikwazo maafisa wa China


Rais Donald Trump

Msemaji wa Baraza la Usalama wa Taifa Marekani amesema Rais Donald Trump hajafutilia mbali hatua ya kuwawekea vikwazo zaidi maafisa wa ngazi ya juu wa China kutokana na namna walivyoshughulikia suala la Hong Kong.

Trump alisaini sheria ya uhuru wa Hong Kong, Jumanne, inayomruhusu kuwawekea vikwazo na marufuku ya visa maafisa wa China na mashirika mengine ya kifedha yanayo jihusisha na kuiwekea Hong Kong sheria ya usalama wa taifa.

Jarida la Bloomberg lilikuwa limeripoti rais Trump alikuwa amesitisha hatua ya kuwawekea vikwazo zaidi maafisa wa China ili kuzuia mgogoro kati ya Marekani na China.

Miongoni mwa wanaolengwa kuwekewa vikwazo ni pamoja na mkuu wa mji wa Hong Kong Carrie Lam kwa kuunga mkono utekelezaji wa sheria ya usalama.

Wiki iliyopita, Trump aliwawekea vikwazo maafisa kadhaa wa Chama cha Kikomunisti cha China - CCP, kutokana na namna walivyo wadhulumu Waislamu wa Uighur.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG