Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 27, 2024 Local time: 03:43

NATO yawafukuza wanadiplomasia wanane wa Russia


Rais wa Russia Vladimir Putin
Rais wa Russia Vladimir Putin

Umoja wa Kujihami wa Nchi za Ulaya (NATO) inawafukuza wanadiplomasia wanane wa Russia na ina mipango ya kupunguza nusu ya ujumbe wa waangalizi wa nchi hiyo  kwenye muungano wa Magharibi.

Hatua hii imechukuliwa kujibu madai ya harakati mbaya za kijasusi za Russia huko Ulaya, ambazo zimejumuisha mauaji, kujaribu kuua na milipuko, wamesema maafisa wa Ulaya.

Wanadiplomasia hao wameambiwa waondoke Brussels mwishoni mwa mwezi huu.

Nafasi nyingine mbili za kidiplomasia za Russia ambazo sasa ziko wazi katika makao makuu ya NATO hazitaruhusiwa kujazwa, maafisa wa NATO waliiambia VOA.

Kufukuzwa kwa wanadiplomasia wanane wa Russia, kuliripotiwa kwanza na Sky News ya Uingereza, kulishutumiwa haraka na wabunge wa nchi hiyo.

Wabunge hao walisema Kremlin italipiza kisasi, ingawa sio lazima iwe vile vile kwa kutaka kuwafukuza wanadiplomasia wa Magharibi walioko Moscow, lakini wakiweka mazingira ya kuzorota zaidi kwa uhusiano kati ya nchi za Magharibi na Russia na kukumbusha kipindi cha vita baridi.

XS
SM
MD
LG