Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 10, 2022 Local time: 10:50

Polisi wawili wapigwa risasi na kujeruhiwa katika maandamano Marekani


Police wakikabiliana na waandamanaji Jumatano,Sept. 23, 2020, huko Louisville, Ky. wakipinga uamuzi wa mahakamakuwa polisi watatu wazungu waliohusika kwenye tukio hilo hawatashitakiwa kutokana na kifo Breonna Taylor. 

Polisi wawili wamepigwa risasi na kujeruhiwa katika mji wa Louisville, Kentucky Jumatano.

Shambulizi hilo limetokea wakati wa maandamano kufuatia uamuzi wa baraza la mahakama lililopingwa na wanaharakati wa haki za binadamu kuhusiana na kupigwa risasi na kuuwawa kwa mwanamke mweusi Breonna Taylor mwezi machi, wakati polisi wakidai kufanya msako.

Baraza hilo kwenye maamuzi yake lilisema kuwa polisi watatu wazungu waliohusika kwenye tukio hilo hawatashitakiwa kutokana na kifo hicho ingawa mmoja wao amefunguliwa shitaka la kuhatarisha maisha ya majirani.

Uamuzi huo umekuja miezi 6 baada ya Taylor aliyekuwa na umri wa miaka 26 kupigwa risasi mbele ya mpenzi wake wa kiume aliyekuwa na bunduki wakati polisi wakidai kufanya msako dhidi ya dawa za kulevya ndani ya nyumba waliokuwa wakiishi.

Kifo cha Taylor kilitokea wakati maandamano makali yakiendelea kushudiwa kote marekani kulalamikia ubaguzi wa rangi.

Mwezi August, mwana televisheni maarufu Oprah Winfrey aliweka picha ya Taylor kwenye ukurasa wa juu wa jarida lake ikiwa kama ishara za kuunga mkono harakati dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG