Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 15:41

Juhudi za kubadilisha mfumo kandamizi wa polisi zaendelea Marekani


Waandamanaji wakiwa mbele ya White House mjini Washington, DC kulaani vitendo vya kikatili na ubaguzi vinavyofanywa na baadhi ya polisi Juni 10, 2020.
Waandamanaji wakiwa mbele ya White House mjini Washington, DC kulaani vitendo vya kikatili na ubaguzi vinavyofanywa na baadhi ya polisi Juni 10, 2020.

Maandamano yamendelea kwa siku ya 16 mfululizo Jumatano ingawa waandamanaji walikuwa wachache kabisa katika miji kadhaa ya hapa Marekani huku juhudi zikiendelea kujaribu kuleta mabadiliko katika mfumo wa sheria na polisi.

Kwa upande mwngine watu wamekuwa wakivunja sanamu na alama zote zinazowakilisha ubaguzi wa rangi na ukoloni hapa Marekani na hata Ulaya.

Wakati maandamano yakiwa yamepungua sana kasi hapa Marekani waandamanaji Jumatano waliendelea kubomboa, kuharibu na kuvunja vichwa vya sanamu ya Christopher Columbus kuanzia miji ya Boston upande wa kaskazini hadi Miami huko kusini.

Vitendo hivyo viliambatana wito wa kuondolewa alama zote zinazowakilisha wakoloni na wamiliki utumwa baada ya maandamano yaliyochochewa na kifo cha George Floyd wiki tatu zilizopita.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi ametaka kuondolewa kwa sanamu kubwa 11 za wanajeshi na maafisa wa enzi ya vita vya wenyewe kwa wenyewe hapa Marekani mwaka 1861 hadi 1865.

Wito wake umetolewa wakati bunge lilikuwa linasikiliza pia mapendekezo ya mageuzi katika vikosi vya polisi ambapo kaka yake George Floyd, Philonise amewarai wabunge kusikia kilio cha wananchi cha kutaka mageuzi.

Philonise Floyd

"Tafadhali sikilizeni wito ninaotoa hapa, wito wa familia zetu, wito unaosikika barabarani kote duniani. Watu wa tabaka zote, jinsia zote na rangi zote wameungana kuomba mageuzi," amesema Philonise.

Juhudi za kondowa alama za ukoloni na ubaguzi zimefanyika katika nchi kadhaa za dunia huko Nairobi Kenya sanamu ya malkia Victoria imebomolewa na Samuel Obiero mkazi wa mji huo anasema sanamu hizi za kikoloni zinabidi kuondolewa kote duniani.

Samuel Obiero Mkazi wa Nairobi anaeleza: Sanamu hii inanikumbusha machungu na tabu zilizo wakumba mababu zetu chini ya mikono ya wakoloni na kila mara tunapozitizama tunakumbushwa maovu waliotendewa. Ndio maana tunahitaji kuziondowa kote duniani.

Masanamu yameondolewa pia, Uholanzi, Ubelgiji na Uingereza ambapo pia kuna majadiliano juu ya kuondolewa sanamu mbalimbali zinazo kumbusha enzi za ukoloni na utumwa.

Huko Palestina kwenye Ukingo wa Magharibi katika mji wa Bethlehem mchoraji asiyejulikana amechora picha kubwa ya George Floyd kwenye ukuta unaowatengenisha na Israel. Kwa Wapelstina wengi kama Hani Al-Halabi mjumbe wa chama cha vijana wa Palestina, kifo cha Floyd kinawakumbusha vita vyao vya uhuru.

Al-Halabi, Mwanachama wa chama cha vijana wa Palestina amesema : "Tunatoa wito kwa taasisi za kimataifa, mashirika ya haki za binadamu na nchi zote huru kutoa heshima zao kwa George Floyd na Mpalestina Iyad Hallak na kuwachukulia ni mashujaa wa kupigania uhuru na ubinadamu katika kiwango cha kimataifa.

Kwa upande wake Rais Donald Trump amepanga kukutana na viongozi wa kidini, maafisa wa Polisi na wamiliki wa biashara ndogo ndogo hii leo Alhamisi huko Dallas wakati anatafakari juu ya namna ya kujibu matakwa ya waandamanaji yaliyofuatia kifo cha George Floyd.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Abdushakur Aboud, Washington, DC

XS
SM
MD
LG