Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 18:02

Trump awania tena urais baada ya kusalimika kuondolewa madarakani


FILE - President Donald Trump Akizungumza wakati wa kampeni mjini Charlotte, Jimbo la North Carolina, Machi 2, 2020.
FILE - President Donald Trump Akizungumza wakati wa kampeni mjini Charlotte, Jimbo la North Carolina, Machi 2, 2020.

Donald J. Trump, Rais wa 45 wa Marekani ni rais wa tatu kufunguliwa mashtaka kutaka kumuondoa madarakani lakini hatimaye akakutwa hana makosa. Anawania tena kuchaguliwa muhula mwingine katika uchaguzi wa Novemba.

Trump alizindua rasmi kampeni yake ya kutaka kuchaguliwa tena mwezi Juni 2019 huko Orlando, Florida, kwa kauli mbiu, “Iendeleze Marekani kuwa yenye nguvu,” ambayo inatofautiana na ile ya mwaka 2016 yenye kauli mbiu “Ifanye Marekani iwe yenye nguvu tena.” Amewaambia wafuasi wake, “Tulifanikiwa mara ya kwanza na hivi sasa tutafanikiwa tena na mara hii tutamaliza kazi.”

Mafanikio ya siku za nyuma :

Kabla ya kuwa rais, Trump alikuwa ni mtu maarufu na pia mfanyabiashara wa majumba huko New York na nyota wa televisheni.

Mara baada ya kuhitimu masomo kutoka Chuo cha Fedha katika Chuo Kikuu cha Pennsylvania, alisimamia biashara ya nyumba, na kuipanua na kujenga hoteli, majumba ya kamari na viwanja wa golf sehemu mbalimbali duniani.

Mwanzoni mwa miaka ya 1990, Trump alilazimika kutangaza amefilisika katika biashara kadhaa ikiwemo mali kadhaa alizokuwa anamiliki huko Atlantic City na New York. Lakini, baadae akaweza kuzijenga tena biashara zake na mwaka 2016, jarida la Forbes lilikadiria utajiri wake unathamani ya dola za Marekani bilioni 3.7.

Mnamo mwaka 2004, Trump akawa anajulikana kote kuwa ni nyota wa vyombo vya habari kwa kutengeneza na kuendesha kipindi cha televishini “The Apprentice,” ambacho kiliipa umaarufu kituo cha televisheni cha NBC. Aliacha kuendesha kipindi hicho mwaka 2015 wakati akijiandaa kugombea urais.

Urais wa Trump: Katika miaka mitatu na nusu ya utawala wake, Rais Trump amepitisha mswaada wa mageuzi makubwa ya kodi, amepunguza vikosi vya jeshi la Marekani nchini Syria, na kushinda kuthibitishwa na baraza la Senate wateule wake wawili katika Mahakama ya Juu , ambaye ni Neil Gorsuch na Brett Kavanaugh wenye misimamo ya sera za Warepublikan, kujaza nafasi katika jopo la majaji tisa wa mahakama hiyo.

Pia alifanikiwa kuthibitishwa kwa takriban majaji wengine 200 katika mahakama za chini za serikali kuu. Uteuzi wa Kavanaugh ulithibitsha kuwepo utata, wakati mahojiano yakilenga ulevi wake siku za ujana wake na madai ya utovu wa nidhamu wa kingono.

Hatimaye, Baraza la Seneti lilipitisha uteuzi wa Kavanaugh katika mahakama ya Juu ya nchini.

Rais Donald Trump baada ya Seneti kumkuta hana hatta, Februari 6, 2020. REUTERS
Rais Donald Trump baada ya Seneti kumkuta hana hatta, Februari 6, 2020. REUTERS

Trump ameweka shinikizo kusukuma mbele sera mbalimbali za kuwakamata wahamiaji wasio halali, ikiwemo ushindi wa kupitishwa kwa takriban dola za Marekani bilioni 1.4 kutoka Bungeni kwa ajili ya ujenzi wa ukuta mpakani (japokuwa ilikuwa kiwango cha chini zaidi kuliko kile alichoomba) na kutangaza hali ya dharura ili kuwezesha dola milioni 3.6 kuidhinishwa zaidi kwa ajili ya ujenzi wa ukuta huo.

Rais huyo ametekeleza baadhi ya ahadi za kampeni kwa kusitisha kanuni za serikali na kufuta sehemu kubwa ya sheria ya matibabu ya afya ya rais mstaafu Barack Obama, maarufu kama Obamacare.

Hata pale ambapo mamilioni ya Wamarekani wamepoteza ajira zao na bima ya afya wakati janga la virusi vya corona lilipoenea duniani kote na kuikumba Marekani mwaka 2020, Trump alikata rufaa Mahakama ya Juu kutengua bima ya afya ya Obamacare kwa ujumla wake.

Trump mara nyingi amekuwa akieleza kutofurahishwa kwake na sera za Obama, mtangulizi wake kutoka chama cha Demokratik na mtendaji mkuu Marekani Mweusi pekee nchini Marekani.

Kwa miaka mitatu, Trump alisimamia uchumi uliostawi ikiwemo kushuka kwa ajira hadi asilimia 3.5, kiwango cha chini zaidi kwa uchumi mkubwa sana duniani kwa miongo mitano, na vipimo vya hisa kuu za Marekani kustawi.

Lakini mafanikio yote hayo yalifikia kikomo bila ya onyo wakati janga la virusi vya corona lilipoenea kuanzia China hadi nchi nyingine duniani mapema 2020, huku Trump akieleza mfululizo mashaka yake juu ya hatari za maambukizi yake na athari zake kwa Marekani,

Mwishoni mwa mwezi februari, katika rekodi ya televisheni iliyokuwa inarejewa katika kipindi cha habari, Trump alitabiri, “virusi vitapotea. Siku moja kama vile miujiza, vitapotea.”

Badala yake, virusi hivyo vilienea katika majimbo yote 50 ya Marekani, na kusababisha taharuki kubwa. Mara taifa zima limekumbwa na balaa la kiuchumi pia.

Zaidi ya wafanyakazi 48 milioni walipoteza ajira zao – zaidi ya robo ya nguvu kazi ya Marekani – wakati magavana wa majimbo wakiamrisha biashara kufungwa katika juhudi za kudhibiti virusi hivyo visienee. Mashule na vyuo vikuu vilisitisha masomo ya darasani na kuamua masomo yafundishwe kwa njia ya mtandao wanafunzi wakisoma kutoka majumbani.

Ligi za soka za kulipwa na vyuo zilisimamishwa, wakati mahospitali yaliahirisha tiba za upasuaji na migahawa ililazimika kuanzisha huduma kwa wateja kuchukua chakula wakisimama nje ya migahawa na katazo la kutokula ndani ya migahawa lilitekelezwa sehemu kubwa ya Marekani.

Trump alianzisha mkutano na wana habari kutoa muhtasari juu ya maambukizi ya virusi vya corona kwa wiki kadhaa, lakini mara nyingi alikuwa akitilia mashaka hatari ya virusi vya corona, inawezekana akihofia kukubali kwa namna yoyote athari zake zitamharibia nafasi yake ya kuchaguliwa tena katika uchaguzi wa Novemba 3.

Aliahidi mara kwa mara kuwa chanjo kwa ajili ya virusi hivyo itapatikana katika miezi ijayo hata pale wataalam wa afya waliposema kuwa chanjo ya umma itapatikana mapema mwaka 2021.

Kwa muda fulani, Trump alijigamba dawa ya kutibu malaria hydroxychloroquine ni tiba kamili ya virusi vya corona na kusema yeye mwenye aliitumia.

Lakini tafiti za afya katika nchi kadhaa zilionyesha haiwezi kutibu virusi na Trump aliacha kabisa kuizungumzia.

Katika kipindi kingine, aliwashangaza Wamarekani kwa kupendekeza kuwa virusi hivyo vinaweza kutibiwa kwa kunywa kemikali yenye sumu.

Wakati wataalam wa afya wakiwataka Wamarekani kuvaa barakoa kudhibiti maambukizi, Trump alisita, akisema hadhani inaenda na hadhi yake, na kukejeli wale waliokuwa wanavaa barakoa hizo.

Polepole, baada ya wiki kadhaa, idadi ya vifo iliongezeka kufikia zaidi ya watu 131,000 nchini Marekani katikati ya mwaka na idadi ya maambukizi ya virusi vya corona iliongezeka na kufikia zaidi ya milioni 3, idadi kubwa zaidi kuliko nchi nyingine yoyote duniani.

Wataalam wa afya wanatabiri kuwa maelfu ya Wamarekani watakufa katika miezi ijayo.

Wakati idadi ya maambukizi ilisambaa katika majimbo ya Marekani yalioko kaskazini, kumekuwa na maambukizi mapya katika majimbo ya kusini ambako magavana walikuwa wa kwanza kurejesha shughuli za kawaida za kiuchumi na baadae ikabidi waamrisha mabaa na biashara nyingine kufungwa tena.

Kiwango cha ukosefu wa ajira nchini Marekani kilifikia asilimia 14.7 mwezi April, halafu kikashuka kufikia asilimia 11.1 mwezi Juni wakati uchumi ukiongeza takriban ajira milioni 5.

Trump, akijipongeza mwenyewe katika uongozi, amesema siku za mafanikio zaidi zinakuja kwa uchumi wa Marekani katika kipindi cha pili cha 2020 na kuelekea 2021.

Wakati virusi vya corona vikinyemelea kimyakimya maeneo mbalimbali Marekani, Trump alilazimika kukabiliana katika baadhi ya wakati na maandamano yenye ghasia kufuatia kifo cha mwanaume Mmarekani mweusi Mei 25, George Floyd, aliyekandamizwa akiwa kifudifudi katika mtaa mmoja Minneapolis, Minnesota na afisa wa polisi mzungu alikandamiza goti lake juu ya shingo ya Floyd akiendelea kufanya hivyo hata pale alipokuwa akinung’unika hawezi kupumua.

George Floyd
George Floyd

Trump alituma ujumbe mchanganyiko juu ya ghasia zilizofuatia kifo hicho, akieleza kuunga mkono maandamano lakini pia akisema kupaza sauti mitaani kwamba “Maisha ya Mtu Mweusi yana thamani” ilikuwa “ni ishara ya chuki.”

Alipaza sauti kuunga mkono picha ya videoya mmoja wa wafuasi wake kisiasa aliyenadi, “Nguvu za wazungu!”

Lakini aliifuta video hiyo kutoka katika akaunti yake ya Twitter baada ya wakosoaji wake kupaza sauti dhidi yake, wakati wasaidizi wa Trump wakisema alikuwa hajasikia kauli ya ubaguzi iliyokuwa katika video hiyo.

Wakati Marekani ikisheherekea miaka 244 ya uhuru wakati wa wikiendi ya Julai 4, Trump aliibuka na hamasa za kisiasa, akipinga waandamanaji wanaodai haki sawa kwa wote ni wawakilishi “waovu” wa “mafashisti wapya wa mrengo wa kushoto” ambao lengo lao la mwisho “kuiangamiza Marekani.”

Kutokana na mabadiliko mbalimbali katika kipindi cha miezi sita ya kwanza ya 2020, hatma ya kisiasa ya Trump ilikuwa haijulikani kwa uhakika, wakati kura za maoni mbalimbali kitaifa zikimuonyesha akiwa nyuma ya Makamu wa Rais mstaafu Joe Biden kwa pointi asilimia 9 miezi minne kabla ya uchaguzi wa rais.

Lakini ni marais wa Marekani wawili tu waliopoteza nafasi ya kuchaguliwa tena katika miongo minne iliyopita na wafuasi wa Trump waligusia kuwa yeye pia ameachwa nyuma katika kura za maoni kabla ya uchaguzi wa 2016, na bila ya kutarajiwa alimshinda Waziri wa Zamani wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton.

Sera ya Mambo ya Nje : Sera ya mambo ya nje ya Trump imetafsiriwa na ajenda yake ya “Marekani Kwanza” ambapo ameweka kile anachoamini kuwa maslahi ya Marekani ni juu kuliko kitu kingine chochote.

Aliiondoa Marekani kutoka katika mikataba kadhaa ya kimataifa ikiwemo ule wa Trans-Pacific Partnership, makubaliano ya kibiashara; mkataba wa hali ya hewa Paris na makubaliano ya nyuklia na Iran.

Kwa upande wa biashara, Trump alitekeleza ahadi ya kampeni aliyoitoa atafanya tena mashauriano ya Makubaliano ya Biashara Huru Amerika Kaskazini na Canada na Mexico, wakati akianzisha mapambano ya kibiashara na China.

Amerejea mara kadhaa kuhoji kiwango cha fedha kinachotumiwa na Marekani kuzihami nchi nyingine na waziwazi ameikosoa NATO, umoja wa kijeshi wa Magharibi ulioanzishwa baada ya vita vya pili vya dunia.

Rais huyu amekuwa na mahusiano mabaya na viongozi wengi wa kigeni, ikiwemo washirika wa siku nyingi kama vile Chansela wa zamani wa Ujerumani Angela Merkel na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.

Lakini amewakumbatia maadui wa kihistoria kama vile Rais wa Russia Vladimir Putin na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un.

Trump alimwita Kim “ mtu wa kombora dogo” lakini baadae alikutana naye katika matukio matatu na kutangaza “ tumeanzisha mahusiano mazuri kati yetu.”

Changamoto za Urais : Trump, mbali na matatizo ya virusi vya corona na uchumi mwaka 2020, amekabiliwa na changamoto nyingi kubwa kama rais, ikiwemo kushtakiwa ili kuondolewa madarakani.

Wademokrat walianzisha mashtaka hayo kutokana na madai kuwa Trump aliiomba Ukraine imsaidie kuchunguza taarifa za kijinai dhidi ya Makamu wa Rais mstaafu Joe Biden na mtoto wake, Hunter Biden, ambazo zingeweza kumuathiri Biden fursa ya ushindi katika kinyang’anyiro cha uchaguzi atakapo jaribu kupambana na Trump 2020.

Makamu wa Rais wa zamani Joe Biden na mwanawe Hunter Biden
Makamu wa Rais wa zamani Joe Biden na mwanawe Hunter Biden

Baraza la Wawakilishi linalodhibitiwa na Wademokrati lilimfungulia mashtaka ya kumuondoa madarakani mwisho mwa 2019, lakini Baraza la Seneti chini ya udhibiti wa Warepublikan halikumuondoa madarakani mapema 2020, ni seneta Mrepublikan mmoja tu aliyepiga kura kuwa ana makosa na aondolewe madarakani.

Trump alikabiliwa pia na uchunguzi wa takriban miaka miwili uliongozwa na mwendesha mashtaka maalum Robert Mueller, ambaye alichunguza Russia kuingilia kati uchaguzi wa 2016.

Mwendesha Mashtaka Maalum Robert Mueller
Mwendesha Mashtaka Maalum Robert Mueller

Ripoti ya mwisho ya Mueller ilithibitisha kuwa kampeni ya Trump haikushirikiana na Russia kuhujumu matokeo ya kinyang’anyiro hicho.

Hata hivyo haikufikia hitimisho lolote iwapo Trump afunguliwe mashtaka ya kuzuia sheria kufuata mkondo wake katika nyakati mbali mbali, inawezekana alijaribu kuzuia uchunguzi wa Mueller.

Katika hali yoyote ile, kuna utamaduni wa muda mrefu unaofuatwa nchini Marekani marais walioko madarakani hawawezi kufunguliwa mashataka ya jinai wakati wakiwa madarakani.

XS
SM
MD
LG