Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 25, 2024 Local time: 22:01

Michelle Obama akosoa utawala wa Trump wakati wa kufungua mkutano mkuu wa Democrat


Wazungumzaji wakuu kwenye ufunguzi wa mkutano wa Democratic, Michelle Obama, Seneta Bernie Sanders, na John Kasich Gavana wa zamani wa Ohio.
Wazungumzaji wakuu kwenye ufunguzi wa mkutano wa Democratic, Michelle Obama, Seneta Bernie Sanders, na John Kasich Gavana wa zamani wa Ohio.

Michelle Obama, mke wa rais wa zamani, amemsifu mgombea mteule wa chama cha Demcratic Joe Biden, kama mtu mwenye uwezo wa kuliongoza taifa, huku akimkosoa vikali Rais Donald Trump kwa kushindwa kufahamu hisia za wengine.

Akiwa wa mwisho kuzungumza katika ufunguzi wa mkutano wa kipekee wa chama cha Democratic, mke wa rais wa zamani Barack Obama alitoa hoja kali kuhusu jinsi Trump ameshindwa kukabiliana na mizozo ya kiuchumi na kijamii pamoja na janga la virusi vya corona hapa nchini.

Mkutano mkuu wa Democrat
Mkutano mkuu wa Democrat

Katika hotuba yake iliyorikodiwa kabla ya Biden kumteua Kamala Harris kuwa mgombea mwenza wake, Bi. Obama amemsifu mgombea huyo kuwa ni mtu mwenye imani na kusikiliza mawazo ya wengine na ataweza kuiongoza nchi hii vizuri zaidi kuliko kiongozi aliyeko madarakani.

“Namfahamu Joe. Ni mtu mzuri ambaye anaongozwa na imani. Alikuwa makamu rais hodari. Anafahamu nini kinatakiwa kuufufua uchumi, kupambana na janga na kuiongoza nchi yetu.” amesema Michelle Obama.

Katika tukio ambalo si la kawaida katika kipindi hiki cha kipekee, bila ya mikusanyiko ya kijamii na matamasha ya televisheni, Eva Longoria Baston nyota wa Holywood aliongoza kwa ustadi siku ya kwanza ya mkutano.

Mkutano mkuu wa Democrat kupitia mtandao
Mkutano mkuu wa Democrat kupitia mtandao

Kulikuwa na ukumbusho wa mivutano ya ubaguzi ambayo imeligawanya taifa, kuanzia kwa Meya wa Washington DC, Muriel Bowser miongoni mwa wengine.

“Ilikuwa ni hapa kiasi cha wiki chache zilizopita, wamarekani walikuwa wamevalia barakoa na kwa amani na usalama waliandamana kupinga kifo cha George Floyd .” amesema Bowser.

Kulikuwa na shughuli za kawaida za mkutano mkuu, lakini washiriki walikuwa wakihudhuria kwa njia ya mtandao.

Jambo muhimu kwa wademocrat ambao wana matumaini ya kumuondoa Rais Trump madarakani, ni uungaji mkono wa wapenda maendeleo ambao ambao walikuwa katika kampeni pamoja na Seneta wa Vermont Bernie Sanders.

“Tunakabiliwa na mzozo mkubwa wa afya kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 100 na uchumi mbaya ulioanguka tangu kipindi cha kudorora kwa uchumi. Tunakabiliana na mfumo wa kibaguzi na vitisho vikubwa kwa dunia yetu kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Katikati ya yote haya, tuna rais ambaye siyo tu hana uwezo wa kuzungumzia mizozo hii lakini pia anatuongoza katika njia ya utawala wa kiimla.”

Pia lililo muhimu, ni uungaji mkono kutoka kwa warepublican na wapiga kura huru. Gavana wa zamani wa Ohio, John Kasich, ambaye ni Mrepublican anamuunga mkono Biden.

“Mimi ni mrepublican maisha yangu yote, lakini hilo hivi sasa liko katika nafasi ya pili kwa wajibu wangu kwa nchi hii. Nimechagua kuonekana kuja katika mkutano huu.”

Chini ya miezi mitatu kabla ya uchaguzi, changamoto kwa vyama vyote, ni kujenga hamasa kwa wagombea wakati huu wa janga la corona.

XS
SM
MD
LG