Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 30, 2022 Local time: 16:40

Polisi Uganda wamegundua kituo cha itikadi kali za kiislam


Polisi wa Uganda

Polisi wa Uganda waligundua bila ya kutarajia “kituo chenye wafuasi wenye kufuata itikadi kali za kislamu” kwenye msikiti mmoja mjini Kampala na kuwauwa watu wawili, na wamewakamata darzeni ya watu pamoja na kuwaachia zaidi ya wanawake na watoto 100, maafisa walisema Jumamosi.

Kulingana na taarifa ya shirika la habari la AFP, chanzo kimoja cha usalama kikizungumza kwa sharti la kutotajwa jina kilisema maafisa waligundua kile kilichoonekana kuwa kituo cha kuelimisha watu kufuata itikadi kali za ki-Islam ndani ya msikiti. Ugunduaji huo ulifanyika Ijumaa wakati maafisa polisi walipomfuatilia mshukiwa mmoja anayeaminika kuhusika katika utekaji nyara na mauaji ya maafisa wa juu mwanzoni mwa mwaka huu, ndani ya msikiti wa mji huo unaofahamika kama Usafi.

Wakati wa majibizano ya risasi, polisi ilisema ofisa polisi mmoja alijeruhiwa, wanaume wawili walifyatuliwa risasi na kuuwawa na 36 walikamatwa na walishukiwa kuwa na silaha. Pia ndani ya msikiti huo kulikuwa na wanawake 18 pamoja na watoto 94 ambao polisi walisema walishikiliwa bila ya ridhaa yao.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG