Picha hizo zimetolewa baada ya wanajeshi wa Russia kuondoka sehemu hiyo.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Michelle Bachelet, amesema kwmaba kuna uwezekano kwamba kulitokea uhalifu wa kivita, kukiukwa kwa sheria ya kimataifa na haki za kibinadamu.
Maafisa wa Ukraine katika mji wa Bucha wamesema kwamba wamelazikika kuchimba makaburi ya pamoja ili kuzika miili kadhaa ya watu waliouawa na kuzuia miili hiyo kujazana barabarani.
Baadhi ya watu waliouawa walikuwa wamefungwa mikono.
Mwendesha mashtaka mkuu wa Ukraine Lryna Venediktova amesema kwamba zaidi ya miili 410 imepatikana kufikia sasa.
Ofisi ya haki za kibinadamu ya umoja wa mataifa imesema kwamba maafisa wako katika sehemu hiyo ya tukio kuthibitisha idadi ya watu waliouawa.