Uturuki imeimarisha juhudi zake za kidiplomasia baada ya kile kimetajwa kama kupatikana mafanikio fulani katika mazungumzo ya jumanne.
Bila kutoa maelezo zaidi, ofisi ya rais wa Ukraine imesema kwamba maafisa wa Russia na Ukraine wamefanya mazungumzo kwa njia ya video.
Katika mahojiano ya televisheni, waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu, amesema kwamba juhudi zinaendelea kuchukuliwa kutatua vita vya Ukraine, akisema kwamba Russia imekubali baadhi ya mapendekezo ya kusitisha vita japo haijatekeleza ahadi hiyo.
Amesema kwamba anaendeela kuwasiliana na mawaziri wa nchi za nje wa nchi hizo mbili kuhakikisha kwamba vita hivyo vinasitishwa.