Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 08:32

Papa Francis ataka ulimwengu kuonyesha huruma zaidi kwa wakimbizi


Pope Francis akiwa ziarani nchini Malta
Pope Francis akiwa ziarani nchini Malta

Kiongozi mkuu wa Kanisa la Katoliki duniani Papa Francis, katika siku ya pili na ya mwisho ya ziara yake nchini Malta ameomba ulimwengu kuonyesha wema na huruma zaidi kwa wakimbizi. Francis alisema hayo wakati alipokutana na wahamiaji nchini humo.

Alizungumza alipotembelea pango la Mtakatifu Paulo mjini Rabat, ambako inaaminika kuwa mitume wa Yesu Kristo walikaa kwenye pango hilo baada ya meli yao kupata hitilafu wakiwa njiani kuelekea Roma.

Kiongozi huyo wa kidini ametumia ziara hiyo kusisitiza tena wito wake kwa Ulaya kuonyesha ukarimu sawa, kwa wahamiaji na wakimbizi, hususan wale wanaokimbia vita nchini Ukraine.

Kwa muda mrefu Malta imekuwa ikishutumiwa juu ya sera yake ya wakimbizi. Taifa hilo lenye jumla ya watu nusu milioni, mara kwa mara imekosolewa na mashirika ya misaada ya kibinadamu kwa kukataa kuruhusu meli za uokoaji kutia nanga kwenye bandari zake, na ujumbe wa Papa Francis unatazamwa na wachambuzi kama uliolenga uongozi wa nchi hiyo, hata kama siyo kwa njia ya moja kwa moja.

Awali Baba Mtakatifu alishiriki misa mjini Florina, na kusema kwamba Yesu watu wanaweza kubadilisha mienendo na mwelekeo wao, kwa sababu Yesu Kristo daima hutoa fursa kwa watu kuanza upya maisha yao.

Ziara yake kwenye kisiwa hicho cha Mediterranean, ambayo imemelizika hii leo, ndiyo yake ya 36 katika nchi za nje tangu achukue usukani kuliongoza kanisa hilo, lenye Zaidi ya wafuasi bilioni 1.3.

XS
SM
MD
LG