Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 07, 2023 Local time: 21:08

Tuhuma za mauaji yakiholela zaongeza shinikizo la vikwazo vikali dhidi ya Russia


Wanajeshi wa Ukraine wanamfunga wire maiti ya raia wakiangalia iwapo kuna mtego wa bomu katika eneo ambalo hapo awali lilivamiwa na majeshi ya Russia huko Kyiv, katika viunga vya mji wa Bucha, April 2, 2022.(AP Photo/Vadim Ghirda)

Russia  inakabiliwa na ongezeko la kulaaniwa kimataifa huku kukiwa na  ripoti za uwezekano kuwa majeshi ya Russia yametenda  uhalifu wa kivita katika viunga vya Kyiv vya Bucha na sehemu nyingine nchini  Ukraine.

Russia inakabiliwa na ongezeko la kulaaniwa kimataifa huku kukiwa na ripoti za uwezekano kuwa majeshi ya Russia yametenda uhalifu wa kivita katika viunga vya Kyiv vya Bucha na sehemu nyingine nchini Ukraine.

Katika ujumbe wa Twitter wa Aprili 3, Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel alisema Moscow itakabiliwa “na vikwazo zaidi vya Umoja wa Ulaya.”

Michael alisema “ameshtushwa na picha za ukatili uliotendwa na majeshi ya Russia huko Kyiv mkoa ambao umekobolewa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Liz Truss alisema katika taarifa yake kuwa serikali yake imeona “ongezeko la ushahidi wa vitendo vya kuhuzunisha vilivyofanywa na majeshi ya uvamizi katika miji kama vile Irpin na Bucha.”

FILE PHOTO: Waziri wa Mambo ya Nje Liz Truss. REUTERS/Tom Nicholson/File Photo
FILE PHOTO: Waziri wa Mambo ya Nje Liz Truss. REUTERS/Tom Nicholson/File Photo

Meya wa Bucha Anatoly Fedoruk alisema Aprili 2 kuwa kiasi cha raia 300 katika eneo hilo walipigwa risasi wakati mji huo ulipokuwa unakaliwa kimabavu na majeshi ya Russia. Watu wapatao 280 wanadaiwa kutupwa

Picha za video na zisizo za video za miili ya watu hao zimesambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

“Kutakuwa na hatua zitakazo chukuliwa kwa uvamizi wa Russia,’ Fedoruk amekaririwa akisema.

Russia haijajibu ripoti hizo.

Vitali Klitschko, Meya wa Kyiv (VOA)
Vitali Klitschko, Meya wa Kyiv (VOA)

Meya wa Kyiv Vitali Klitschko ameliambia gazeti la Ujerumani Bild kuwa “ kile kilichotokea huko Bucha na viunga vya Kyiv kinaweza tu kuelezewa kama ni mauaji ya kimbari.” Amesema Rais wa Russia Vladimir Putin anawajibika.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dymtro Kuleba alisema kuwa” mauaji ya Bucha yalifanywa kwa makusudi.”

“Ninataka vikwazo vipya vikali viwekwe hivi na G7,” Kuleba aliandika Aprili 3 katika Twitter, akielezea kundi hilo la nchi saba zenye uchumi unaongoza duniani.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG