Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 05:19

Ukraine yasema tayari imeudhibiti mji mkuu, Kyiv na maeneo yanayo uzunguka

Mwanajeshi wa Ukraine akiwahami wanajeshi wenzake waliokuwa wanarejea nyuma baada ya kuikagua miili iliyokuwa barabarani baada ya wanajeshi wa Russia waliokuwa hapo awali wamevamia eneo la vijijini la Bucha, mji mkuu wa Kyiv, April 2, 2022. (AP Photo/Vadim Ghirda)

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameonya kuwa kile Russia ilichoacha nyuma huko Kyiv na katika maeneo  jirani ni “janga kamili,” eneo la ardhi, nyumba na vifaa vilivyotegewa mabomu. Rais anadai kuwa hata miili ya watu waliokufa imetegeshewa mabomu.

Ukraine imesema Jumamosi imeudhibiti mji mkuu Kyiv na maeneo yanayouzunguka, wakati majeshi ya Russia yakiondoka.

Maafisa wa ujasusi na ulinzi wa Marekani na wa Magharibi wametahadharisha kuwa Moscow inayahamisha majeshi yake kwa maandalizi ya kile Kremlin ilichosema itakuwa ni dira mpya kwa mkoa wa Donbas huko mashariki mwa Ukraine.

Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa Ukraine “imekamata tena zaidi ya miji na vijiji 30 kuzunguka Kyiv.”

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameonya kuwa kile Russia ilichoacha nyuma huko Kyiv na katika maeneo jirani ni “janga kamili,” eneo la ardhi, nyumba na vifaa vilivyotegewa mabomu. Rais anadai kuwa hata miili ya watu waliokufa imetegeshewa mabomu.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy akizungumza na Rais wa Bunge la Umoja wa Ulaya Roberta Metsola huko Kyiv, Ukraine, April 1, 2022.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy akizungumza na Rais wa Bunge la Umoja wa Ulaya Roberta Metsola huko Kyiv, Ukraine, April 1, 2022.

Zelenskyy alisema Jumamosi katika hotuba yake usiku, “Tusijifariji na matumaini matupu kuwa” Warussia hao “ wataondoka tu katika ardhi yetu.” Alisema amani inaweza kupatikana tu kwa “mapigano makali,” “mashauriano” na “ari ya kazi kila siku”

Ripoti kutoka Odesa, kuhusu pwani ya Ukraine ya Black Sea, iznasema shambulizi la kombora la Russia katika kiwanda cha kusafisha mafuta cha Odesa limeharibu kiwanda hicho.

Wizara ya Ulinzi ya Russia imesema katika taarifa yake, “Asubuhi ya leo, makombora kutoka baharini na angani yenye uwezo wa kulenga bila ya kukosa yameharibu kiwanda cha kusafisha mafuta na ghala tatu za petroli na mafuta karibu na mji wa Odessa, ambako mafuta yanasambazwa kwa kundi la wanajeshi wa Ukraine.

Shirika la ujasusi ndani ya jeshi la Uingereza lilisema Jumapili kuwa mabomu yaliyoripotiwa eneo la Black Sea ni hatari kubwa kwa shughuli za baharini. Shirika hilo limesema chanzo cha mabomu hayo yanazozaniwa na hakiko wazi lakini kuna uwezekano mkubwa itakuwa ni kazi ya jeshi la Russia.

Kushoto, Rais wa Russia Vladimir Putin na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy.
Kushoto, Rais wa Russia Vladimir Putin na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy.

Mkuu wa upande wa Ukraine katika mazungumzo ameashiria, hata hivyo, kuwa mazungumzo kati ya Zelenskyy na Rais wa Russia Vladimir Putin yanaweza kufanyika baada ya “wapatanishi wa Moscow katika mazungumzo kukubaliana kusiko rasmi kwa rasimu ya mapendekezo karibuni yote yaliyojadiliwa wakati wa mazungumzo ya ana kwa ana huko Istanbul” wiki iliyopita, kulingana na ripoti za shirika la habari la AP.

XS
SM
MD
LG