Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 07:27

Norway : Mshukiwa wa shambulizi la msikitini akataa kutoa ushirikiano


Wafanyakazi wa huduma ya dharura wakiwa karibu na kitanda cha kubebea majeruhi baada ya shambulizi la bunduki katika kituo cha msikiti wa al-Noor, karibu ya Oslo, Norway Agosti 10, 2019. NTB Scanpix/Terje Pedersen via REUTERS
Wafanyakazi wa huduma ya dharura wakiwa karibu na kitanda cha kubebea majeruhi baada ya shambulizi la bunduki katika kituo cha msikiti wa al-Noor, karibu ya Oslo, Norway Agosti 10, 2019. NTB Scanpix/Terje Pedersen via REUTERS

Wakili wa mshukiwa wa jaribio la shambulizi katika msikiti moja karibu na mji mkuu wa Oslo, Norway, amesema mteja wake amepinga kutoa ushirikiano wowote kwa wachunguzi wa tukio hilo mwisho wa wiki.

Mshukiwa huyo Philip Manhaus raia wa Norway, 21, alifikishwa mahakamani nchini humo akionekana amejeruhiwa jicho moja huku akiwa anatabasamu.

Mtu huyo anakabiliwa na mashtaka ya mauaji na jaribio la mauaji. Hakuna mtu aliyeuwawa ndani ya msikiti huo, lakini saa chache baadae polisi waligundua maiti ya dada wa kambo wa mshukiwa katika eneo jingine na anatuhumiwa kwa mauaji hayo.

Polisi ya Norway inaliangalia tukio hilo la Jumapili la mtu huyo kutaka kushambulia kwa risasi msikiti huo kama jaribio la kigaidi.

Naibu Mkuu wa Polisi wa mji wa Oslo Rune Skjold amesema polisi wamepata ushahidi kuwa mshukiwa alikuwa na maoni makali ya mrengo wa kulia, na inashukiwa kwamba alikuwa na chuki dhidi ya wahamiaji.

Jumapili, mshukiwa alianza kuwarushia risasi watu wawili kwenye msikiti huo, lakini baadae alidhibitiwa na mzee wa miaka 65 ambaye ni afisa wa zamani katika jeshi la anga la Pakistani.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG