Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 08:28

Shambulizi la Msikitini New Zealand : Watu nchini na nje ya nchi washiriki maziko


Watu wakisubiri kutoa heshima zao za mwisho kwa miili ya marehemu waliouawa katika shambulizi la New Zealand.
Watu wakisubiri kutoa heshima zao za mwisho kwa miili ya marehemu waliouawa katika shambulizi la New Zealand.

Jeshi la polisi New Zealand limeendelea kushirikiana na familia mbalimbali kuweza kufanikiwa kuwatambua wahanga wa shambulizi la siku ya Ijumaa katika misikiti miwili ilioko mjini Christchurch, wanajamii walizika miili ya baadhi ya watu wao Jumatano na wanajaribu kuendelea mbele na maisha yao.

Mwandishi wa VOA anaeleza kuwa Jumatano ilikuwa siku ya shughuli nyingi katika mji wa Christchurch, New Zealand, siku tano baada ya shambulizi lenye maagamizi makubwa kuwaathiri wanajamii, na kusababisha vifa vya watu 50 katika wanajumuia wa misikiti hiyo miwili Ijumaa iliyopita.

Wakimbizi wawili kutoka Syria, baba na mtoto, walizikwa katika uwanja wa kumbukumbu wa mji huo, Memorial Park. Mazishi hayo yalihudhuriwa na mamia ya watu, baadhi yao walikuwa wamesafiri kutoka mji wa Invercargill – nikiwa Imam nimeongea mapema leo na wale waliyokuja kusaidia familia kuandaa ibada ya maziko, na pia Waislam wengine kutoka nchi mbalimbali duniani.

Kamishna wa polisi wa New Zealand Mike Bush amesema kuwa kutambua miili ilioyosalia na kuikabidhi kwa familia zao ili waweze kuandaa mazishi, inabakia kuwa ni kipaumbele chetu.

“Mchakato wa kuwarejesha wahanga kwa familia zao zenye upendo mkubwa, hili kwetu sisi ni kipaumbele kilicho wazi – kwa sababu mbalimbali za kifamilia, kwa sababu mbalimbali za upendo wao na kwa sababu za utamaduni. Mchakato huo unaendelea vizuri sana, ilikuwa ni dhamiri yetu kufanya kila tunaloweza kukamilisha hilo siku ya leo, hakika tunaendelea kupiga hatua nzuri sana,” amesema Kamishna huyo.

Waziri Mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern alikuwa pia katika mji wa Christchurch leo. Ametembelea shule za eneo hilo. Ujumbe wake kwa wanafunzi ulikuwa wazi – ni sawa kabisa kuombeleza.

“Amesema ni sawa kabisa kuomba msaada, hata kama hujaathiriwa na tukio hili moja kwa moja. Mambo haya, picha hizi ambazo watu wanaziona ni vigumu sana kukabiliana nazo," amesema Waziri Mkuu.

Wakati mji huo ukiendelea kukabiliana na janga hilo na kuzungumzia njia bora ya kuendelea na maisha, kinachojitokeza ni idadi ya ujumbe wa rambirambi na alama za kumbukumbu zinazoendelea kuwekwahapa katika uwanja wa Hagley Park ulioko pembeni ya Msikiti wa al-Noor. Maua na kadi zenye ujumbe wa rambirambi zilizowekwa katika uzio wa mitaa hiyo, iliyoko upande wa uwanja wa Park, ni alama ya kutosha ya kiunganishi cha upendo kati ya wanajamii.

XS
SM
MD
LG