Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 08:57

1 auawa, 3 wajeruhiwa, katika shambulizi la Sinagogi California


Waumini wakipeana pole nje ya Sinagogi Jumamosi, Aprili 27, 2019.
Waumini wakipeana pole nje ya Sinagogi Jumamosi, Aprili 27, 2019.

Mtu mmoja ameuawa na wengine watatu kujeruhiwa na mtu mwenye silaha aliyeingia katika sinagogi Jumamosi huko mjini Poway, Jimbo la California na kuanza kushambulia. Poway iko kilomita 25 kaskazini mwa Jiji la San Diego.

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari, mkuu wa polisi wa Kaunti ya San Diego, Bill Gore amesema mwanaume mmoja mzungu aliingia katika sinagogi kabla kidogo ya kufikia saa tano na nusu asubuhi, majira ya pwani ya magharibi, Marekani, na kuanza kurusha risasi kwa kutumia silaha ya kivita aina ya AR ambayo inawezekana ilipata hitilafu baada ya kurusha risasi kadhaa.

Amesema watu wanne – mwanamke, msichana na wanaume wawili, moja kati yao ni kasisi wa sinagogi hiyo walijeruhiwa kwa risasi.

“Inasikitisha, kwani mmoja kati yao alikufa kutokana na majeraha ya risasi,” Gore amesema. Ameongeza kusema kuwa waathirika wengine watatu, akiwemo kasisi, wako katika hali nzuri.

Wengine waliopatwa na risasi ni Waisraeli wawili – mtoto wa kike wa miaka nane na mjomba wake mwenye umri wa miaka 31. Walihamia San Diego miaka michache iliyopita wakitokea mji karibu na Ukanda wa Gaza, Israeli, ambao uliripotiwa kushambuliwa na roketi.

Gore amesema kuwa afisa wa polisi wa doria mpakani aliyekuwa hayuko kazini ambaye alimuona mtu huyo akikimbia kutoka katika eneo la tukio la uhalifu huo alilenga bunduki kuelekea kwa mshukiwa huyo. Lakini mshukiwa huyo risasi haikumpata na badala yake ilipiga gari.

Mkuu wa Polisi wa San Deigo David Nisleit amesema kuwa mshukiwa huyo ilielekea kuwa aliwasiliana na polisi na baadae akajisalimisha kwa afisa wa polisi San Diego ambaye alikuwa anaelekea katika eneo shambulizi hilo la bunduki lilipotokea.

Amesema mshukiwa huyo ana umri wa miaka 19 na anaishi San Diego.

Nisleit alituma ujumbe wa tweet kuwa kitengo chake kinasaidia katika uchunguzi huo, na kuwa wakati hakuna vitisho vyovyote vilivyotolewa “kwa kuchukua tahadhari ya kutosha, tutatoa ulinzi wa doria wa ziada katika maeneo ya ibada.”

Jumamosi ilikuwa ni siku ya mwisho ya sikukuu ya Wayahudi ikiwa ni kumbukumbu ya kukombolewa kutoka utumwani huko nchini Misri.

XS
SM
MD
LG