Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 12:54

Mashambulizi ya Sri Lanka yahusishwa na mtandao wa kimataifa


Wananchi wa Sri Lankan wanaoishi karibu na eneo la kanisa la St Anthony wamekimbilia eneo salama baada ya polisi kugundua mabomu ndani ya gari iliyokuwa imeegeshwa ambayo iliripuka Colombo, Sri Lanka, Aprili 22, 2019.
Wananchi wa Sri Lankan wanaoishi karibu na eneo la kanisa la St Anthony wamekimbilia eneo salama baada ya polisi kugundua mabomu ndani ya gari iliyokuwa imeegeshwa ambayo iliripuka Colombo, Sri Lanka, Aprili 22, 2019.

Afisa mmoja nchini Sri Lanka amesema kikundi cha ndani cha wapiganaji kikisaidiwa na mtandao wa kigaidi wa kimataifa wanahusika na mashambulizi yaliotokea wakati wa paska Jumapili kwenye makanisa na hoteli nchini humo ambapo watu 290 waliuawa na wengine 500 kujeruhiwa.

Waziri wa afya wa taifa hilo Rajitha Senaratne amesema Jumatatu kundi la National Thowfeed Jamaath wanahusika na mashambulizi hayo.

Ameongeza kuwa, “bila ya mtandao wa kimataifa mashambulizi haya yasingeweza kufanikiwa.”

Senaratne amesema kuwa mashambulizi hayo katika maeneo sita – makanisa matatu na hoteli tatu – yalitekelezwa na watu saba waliojitoa muhanga kwa mabomu. Wote waliojitoa muhanga ni raia wa Sri Lanka, Senaratne amesema.

Shirika la habari la AP linaripoti kuwa washukiwa 24 tayari wamekamtwa kutokana na matukio hayo. Mapema Jumatatu amri ya kutotoka nje imetangazwa kuanzia saa mbili za usiku hadi saa kumi za asubuh

Gari moja lililipuka Jumatatu karibu na kanisa mojawapo ambapo mlipuko ulitokea Jumapili. Polisi walijaribu kulitegua mabomu yaliyokuwa ndani ya gari, laikini mabomu yaliripuka. Hakuna mtu aliyejeruhiwa katika tukio hilo.

Rais wa Sri Lanka Maithripala Sirisena atatangaza hali ya hatari ya kitaifa kuanzia saa sita usiku Jumatatu. Vyombo vya habari vya ofisi ya Rais vimesema hatua hiyo ya dharura itatumika tu kupambana na ugaidi na haitazuia uhuru wa kujielezea.

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa washukiwa 24 wamekamatwa kutokana na milipuko hiyo.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG