Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 16:15

Waislam Sri Lanka wahofia ulipizaji kisasi baada ya mashambulizi makanisani


Wananchi wa Sri Lanka wakishiriki katika mazishi ya wahanga wa mashambulizi kanisani na mahotelini.
Wananchi wa Sri Lanka wakishiriki katika mazishi ya wahanga wa mashambulizi kanisani na mahotelini.

Waislamu wa Sri Lanka wameeleza Jumatano wasi wasi wao juu ya uwezekano wa kutokea ulipizaji kisasi kufuatia mashambulizi ya mabomu wakati wa sikukuu ya Pasaka katika makanisa na hoteli za kifahari Colombia.

Waislamu ambao ni asilimia 10 ya wakazi milioni 21 wa Sri Lanka. Wananchi wa Sri Lanka waliowengi ni kabila la Sinhale wanaofuata dini ya kibuda.

Makamu wa rais wa Baraza la Waislamu wa Sri Lanka amesema tayari wameshuhudia baadhi ya watu wakirusha mawe kwenye misikiti mbali mbali, huku watu wengine wakihama makazi yao kutokana na hofu ya kushambuliwa.

Wakati huohuo Waziri wa Ulinzi wa Sri Lanka anasema idadi ya waliofariki imeongezeka na kufikia 359, na kumetokea mlipuko mmoja wa bomu Jumatano, karibu na jengo la sinema la Savoy, na bomu jingine kupatikana katika mtaa wa biashara wa Colombo.

Katika tukio hilo jipya la mlipuko hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa. Maafisa wa usalama wanasema watu 60 wamekamatwa hadi hivi sasa ili kuhojiwa kutokana na mashambulio hayo ya Jumapili.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Abdushakur Aboud, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG