Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 30, 2023 Local time: 13:38

Ndege ya kwanza yatua Sanaa, Yemen baada ya miaka sita


Ndege ya Shirika la Ndege la Yemen ikirushiwa maji kama salamu za pongezi kwa kuanza safari ya kwanza ya ndege baada ya kusitishwa kwa miaka sita, wakati ilipowasili Uwanja wa Ndege wa Sanaa, mjini Sana'a, Yemen, May 16, 2022.

Ndege ya kwanza ya abiria baada ya takriban miaka sita iliruka kutoka mji mkuu unaoshikiliwa na waasi nchini Yemen Jumatatu, maafisa wamesema, ikiwa ni sehemu ya sitisho la mapigano tete katika nchi hiyo iliyokumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Ndege ya shirika la ndege la Yemenia inayojulikana kama Yemen Airways ilikuwa ikielekea mji mkuu wa Jordan, Amman, kulingana na vyombo vya habari vinavyoendeshwa na waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran.

Mapema ndege hiyo iliwasili Sanaa kutoka mji wa kusini wa bandari wa Aden na kubeba abiria.

Wakati ndege ikitua kulikuwa na sherehe za kuikaribisha, ambapo ofisi ya vyombo vya habari vya kihouthi imesema ilirejea ikiwa na abiria 60 kwenda mji wa Sanaa kutoka Amman baadae Jumatatu.

Raed Teleb Jabal , waziri mdogo wa anga na mamlaka ya hali ya hewa , Sanaa amesema: “Leo, baada ya kusubiri kwa muda mrefu wa miaka sita, uwanja wa ndege wa Sanaa umepokea ndege kutoka shirika la ndege la Yemen kama sehemu ya makubaliano ambapo ndege mbili zilitarajiwa kufanya operesheni zake kwa wiki kwa kipindi cha miezi miwili.

Lakini kwa bahati mbaya, mwezi wa kwanza na nusu ya mwezi wa pili ilivuka na hakukuwa na ndege zozote zilizofanya safari. Leo ndege ya kwanza iliyobeba abiria 137 imefanya operesheni zake kwenda uwanja wa ndege wa Amman nchini Jordan na kurejea na takriban na abiria 60 katika uwanja wa ndege wa Sanaa.”

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG