Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 08, 2023 Local time: 06:26

Rais wa Yemen na naibu wake wajiondoa madarakani


Rais wa Yemen Abed Rabbo Mansour Hadi akihutubia kikao cha 73 cha baraza kuu la umoja wa mataifa Sept 26 2018. PICHA: AP
Rais wa Yemen Abed Rabbo Mansour Hadi akihutubia kikao cha 73 cha baraza kuu la umoja wa mataifa Sept 26 2018. PICHA: AP

Rais wa Yemen Abdrabuh Mansour Hadi ameachia madaraka yake yote na kuliagiza baraza la rais kuongoza nchi hiyo, ikiwemo kusimamia mazungmzo ya kumaliza vita kati ya serikali na waasi wa Kihuthi.

Tangazo la mapema Alhamisi, lililochapishwa na shirika la habari la serikali SABA, limesema kwamba Rashad Al-Alimi, ambaye ni mshauri wa rais Hadi na aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya ndani, ataongoza baraza hilo, lenye wanachama saba.

Hadi vile vile amelipa baraza hilo madaraka ya naibu wa rais, na kuitaja kamati ya wanachama 50 itakayotoa ushauri kwa baraza hilo kuhusiana na juhudi za amani.

Waasi wa kihuthi waliuteka mji mkuu wa Yemen, Sanaa, mwaka 2014 na kupelekea rais Hadi na serikali yake kukimbilia uhamishoni Saudi Arabia.

Saudi Arabia ilianzisha oparesheni za kijeshi zinazounga mkono utawala wa Hadi.

Mapigano ya Yemen yameua zaidi ya watu 150,000 na kuwaacha mamilioni bila makazi, katika mojawapo ya hali mbaya ya kibinadamu duniani.

XS
SM
MD
LG