Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:49

Saudi Arabia na washirika wake watangaza sitisho la mapigano Yemen.


Wanajeshi wa Yemen watiifu kwa serikali inayotambuliwa kimataifa wakipiga doria katika mji wa Marib, Februari 2, 2018.
Wanajeshi wa Yemen watiifu kwa serikali inayotambuliwa kimataifa wakipiga doria katika mji wa Marib, Februari 2, 2018.

Muungano wa ushirika unaoongozwa na Saudi Arabia ambao unaunga mkono serikali ya Yemen katika vita dhidi ya Wahuthi umetangaza Jumanne sitisho la mapigano kuanzia leo Jumatano asubuhi na mazungumzo ya amani wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ambao unaanza mwezi ujao.

“Muungano huo unatangaza kusitishwa kwa operesheni za kijeshi nchini Yemen kuanzia saa kumi na mbili asubuhi Jumatano, Machi 30, 2022,” umesema katika taarifa iliyotolewa na shirika la habari la Saudia.

Taarifa ya muungano huo inakwenda sabamba na kuzinduliwa kwa mashauriano kati ya Wayemen kwa lengo la kujenga mazingira bora kwa ajali ya maafanikio ya mashauriano hayo na kuweka mazingira chanya wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa ajili ya kuleta amani nchini Yemen,” taarifa hiyo imeongeza.

Mjumbe wa Umoja wa mataifa Hans Grundberg mapema Jumanne jioni alisema kwenye Twitter “ Ninashukuru sana kwa uungwaji mkono wa pamoja ulioonyeshwa kwa juhudi za Umoja wa mataifa juu ya upunguzaji wa mara moja na utatuzi wa kisiasa wa mzozo.”

XS
SM
MD
LG