Saudi Arabia ambayo ni mzalishaji na muuzaji mkubwa mafuta ghafi duniani imetangaza kupunguza kwa muda uzalishaji huo katika kiwanda chake kinachosimamiwa na kampuni kubwa ya mafuta ya Aramco baada ya waasi wa Kihuthi kuazisha mashambulizi mpakani.
Shambulizi lililotekelezwa na ndege isiyokuwa na rubani dhidi ya kiwanda cha kusafisha mafuta cha YASREF katika mji wa viwanda wa Yanbu karibu na bahari ya sharma limepelekea kupungua kwa uzalishaji wa mafuta.
Wizara ya Nishati imesema kwamba hakuna matu aliuawa katika shambulizi hilo.
Taarifa ya wizara ya nishati imesema kwamba mashambulizi mawili yaliyotekelezwa na ndege zisizokuwa na rubani, yaligonga viwanda vya Yanbu na YASREF, vinavyozalisha pipa 400,000.
Maafisa wamesema kwamba shambulizi hiyo linafuatia shambulizi kama hilo lililotekelezwa Jumamosi dhidi ya kiwanda cha kusambaza petrol katika mji wa Jizan, kusini mwa nchi hiyo.
Waasi wa Kihuthi, wanaoungwa mkono na Iran, na ambao wanapambana na muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia nchini Yemen, wamekuwa wakitekeleza mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya ufalme huo ikiwemo dhidi ya viwanda vinavyosimamiwa na Aramco.
Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali vya habari.