Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 20:56

Mwanamuziki Haacaaluu Hundeessaa azikwa chini ya ulinzi mkali


Maziko ya mwanamuziki Haacaaluu Hundeessaa mjini Ambo, Ethiopia, Julai 2, 2020.
Maziko ya mwanamuziki Haacaaluu Hundeessaa mjini Ambo, Ethiopia, Julai 2, 2020.

Mazisihi ya muimbaji kutoka kabila la Oromo aliyeuawa mapema wiki hii yamefanyika Alhamisi katika mji wa Ethiopia wa Ambo chini ya ulinzi mkali.

Mauaji ya muimbaji Haacaaluu Hundeessaa yamechochoea maandamano ya siku mbili na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 80.

Sherehe za kuaga mwili wake zilifanyika kwenye uwanja wa Ambo.

Mke wa Haacaaluu, Santu Demisew Diro amesema Haacaaluu hakufa, atabaki katika moyo na masikio ya mamilioni ya wa Oromo milele.

Naomba mnara wa ukumbusho kwa ajili yake ujengwe mjini Addis Ababa, ambako damu yake ilimwagika, ameongeza Demisew Diro.

Matangazo ya moja kwa moja yameonyesha kuwa idadi ya watu kwenye uwanja ilikua ndogo.

Polisi wamewarudisha nyuma watu ili wasifike uwanjani, mkazi mmoja wa Ambo ambaye alijaribu kuhudhuria sherehe hizo, lakini akakutana na umati wa watu ambao waliambiwa warudi nyumbani, ameliambia shirika la habari la Reuters.

Muimbaji huyo aliuawa Jumatatu mjini Addis Ababa na watu wasiojulikana waliokuwa na silaha.

Kifo chake kimesababisha maandamano makubwa mjini Addis Ababa na katika jimbo la Oromia, maandamano ambayo yalipekea zaidi ya watu 80 kuuawa kutokana na milipuko mitatu.

Nyimbo za Haacaaluu zilitumiwa na vijana waandamanaji wa kabila la Oromo katika maandamano dhidi ya serekali ya Ethiopia.

Maandamano ya miaka mitatu dhidi ya serikali yalimlazimisha Waziri Mkuu wa zamani Hailemariam Desalegn kujiuzulu mwaka 2018, baadae akateuliwa Waziri Mkuu wa hivi sasa, Abiy Ahmed ambae nae ni kutoka kabila la Oromo.

XS
SM
MD
LG