Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 06:04

Museveni akataa udhuru wa Burundi


Rais Pierre Nkurunziza
Rais Pierre Nkurunziza

Rais wa Uganda Yoweri Museveni, ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), amekataa kuahirisha kikao cha ishirini cha viongozi wa jumuiya hiyo mjini Arusha, baada ya Burundi kumtaka kufanya hivyo.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, anataka kikao hicho kiahirishwe kwa wiki mbili zaidi, akisema kwamba Burundi haijajitayarisha kushiriki mkutano.

Ajenda kuu ya mkutano huo ni mzozo wa kisiasa wa Burundi, baada ya wawakilishi wa serikali kukosa kushiriki mazungumzo ya amani yaliyo kuwa yakiongozwa na rais mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa, nchini Tanzania.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amependekeza kwamba Burundi inastahili kujipatia katiba mpya, itakayo jumlisha kila mwananchi na kuruhusu raia wake wote waliokimbilia nchi za nje kurejea nyumbani.

XS
SM
MD
LG